Key: 1. RANGI YA NJANO - Njia ya Uelekeo Mmoja {One Way}.
 2. RANGI YA BLUE MPAUKO - Njia ya Mielekeo Miwili {Two Way} 
 3. RANGI YA KIJANI - Mitaa ya Kutembea kwa Miguu Magari marufuku {Walking Streets} 
 4. RANGI NYEKUNDU - Barabara za kupita Daladala
 5. RANGI YA BLUU ILIYOIVA - Barabara za DART
 6. DUARA ZA NJANO - Mzunguuko {Roundabout} 
 7. MSALABA WA KIJANI - Makutano yenye Taa za kuongozea Magari {Singnalized Intersection}
1. Kipande cha Mtaa wa Samora kuanzia Mnara wa Askari (Askari Monument) hadi Clock Tower Magari  kutakuwa na mabadiliko ambayo magari yatakuwa yanaelekea Clock Tower badala ya Askari Monument. 

2. Barabara ya Sokoine kuanzia Station hadi Makutano ya Mtaa wa Maktaba Posta Ya Zamani Magari yatakuwa yanaelekea Uelekeo mmoja wa Station Posta ya Zamani tofauti na ilivyo sasa Posta ya Zamani kwenda Station. 

3. Barabara ya Kivukoni  Kuanzia Posta ya Zamani hadi Ferry itakuwa barabara ya mielekeo miwili (Two Ways).

4. Barabara ya Samora kuanzia Mnara wa Askari hadi Ocean Road Hospitali itakuwa ni barabara ya mielekeo miwili.

5. Daladala Zote zitakazotokea barabara za  Makataba zitakunja kulia pembeni ya Jengo la NBC na hadi Makutano ya Mkwepu na kukunja kushito kuingia Sokoine pale Posta ya Zamani na baadaye kukunja kushoto kuingia Makataba na kurudi Posta Mpya .

Kwa Maelezo zaidi Wasiliana na Ofisi za DART
UBUNGO PLAZA GHOROFA YA KWANZA.
AU.
OFISI YA MHANDISI WA MANISPAA YA ILALA
MABALA NA SHOPRITE SUPEEMARKET JIRANK NA KAMATA

Mtaarifu mwingine juu ya mabadiliko haya kuondoa usumbufu ifikapo siku ya Jumatatu 28/04/2014. PASAKA NJEMA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. CBD haijafafanuliwa. Ningetegemea Central Business District (mjini kati) iwe kwa barabara ya morogoro iwe Bibi Titi, Ya bagamoyo iwe msalaba mwekundu na ya kilwa iwe relwe stesheni si vema kila mmoja akawa namipakayake ya CBD.

    ReplyDelete
  2. Mmeweka vibao vya kuonyesha hivyo lakini ama maneno tu? Wekeni vibao kwanza.

    ReplyDelete
  3. Hii kitu ilitakiwa ifanyike uelimishaji kwa sie tulojaaliwa vipando kwa Muda mrefu na si kuja na order Kama tupo kambini, dart ,jiji na wahusika wengine tunashukuru kwa maboresho na tunaamini yatakuwa yenye tija kwa kuepusha misongamano isiyokuwa na ulazima katikati ya jiji shida ni taarifa imekuwa short notice mno .Tafadhali jipangeni tena or else tutarajie ajali nyingi sana kwa mabadiliko Haya.
    Mungu ibariki Tanzania
    Mungu ibariki Afrika
    Pasaka njema...

    ReplyDelete
  4. Point Nr 4, kwenye ramani haionyeshi hivyo,kwani inaonyesha one way drive towards askari monument!

    ReplyDelete
  5. Nafikiri hili zoezi likifanikiwa huenda likaondoa kabisa foleni mjini

    ReplyDelete
  6. Fikirieni upya point namba 5!! Kutakuwa na vurugu na usumbufu ambao hujawahi kutokea!

    Anayebisha tupinge!! (Shs 1,000/)

    Kunta Kinte

    ReplyDelete
  7. ulaji huooooooo kwa yange yange....

    ReplyDelete
  8. Wekeni alama za kuonesha barabara zinazo onekana na kueleweka. Watu wanaendesha magari kwa uzoefu na si kwa kufuata ramaniza barabara. Hata vialama vichache vilivyowekwa ni vidogo mno. Huwezi kuviona ukiwa umbali fulani. Alama za kuonesha barabara ziwe kubwa kama matangazo ya biashara ili wanaondesha magari weweze kujua zinakoelekea barabara. Si wote ni wenyeji wa Dar. Hata hili mnasubiri tufundishane. Elimu si inatosha!!!

    ReplyDelete
  9. Ni vyema

    ReplyDelete
  10. Supprisingly website ya DART www.dart.go.tz haina information zozote kuhusi hili....Page yao imejaa habari za miezi kadhaa ya nyuma tena zile za kufurahisha 'wakubwa'Bodi members, kamati ya bunge nk....sasa unajiuliza hii site ni ya kazi gani?

    ReplyDelete
  11. Ukitizama ramani na maelezo yaliyotolewa ni tofauti kabisa hasa kwa njia ya daladala pale posta ya zamani. Sasa tufuate maelezo ama ramani? Maana hata vibao sijaviona kwenye njia zilizoelezwa kuwa na mabadiliko.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...