Mshiriki wa Tanzania Movie Talents akihojiwa mara baada ya kumaliza usaili katika Shindano la Tanzania Movie Talents linaloendelea muda huu katika Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo Soko Matola Mkoani Mbeya
 
Baadhi ya washiriki waliojitokeza kwaajili ya kuhudhuria usaili wa Shindano la Tanzania Movie Talents wakijadiliana jambo kabla ya kuanza kwa usaili.
 
 Washiriki waliojitokeza kwaajili ya kushiriki mashindano yya Tanzania Movie Talents wakijaza fomu kwaajili ya usaili wa shindano la Tanzania Movie Talents linaloendelea Mkoani Mbeya ikiwa unawakilisha Kanda ya Nyanda za Juu Kusini
 Baadhi ya washiriki kutoka Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mkoani Mbeya wakisubiri shindano la Tanzania Movie Talents kuanza.
Kundi la Kwanza La vijana waliojitokeza kwaajili ya usaili wa Shindano la Tanzania Movie Talents linaloendelea mkoani Mbeya muda huu.Picha na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Mbeya.

Hatimaye Shindano la Tanzania Movie Talents limeanza rasmi leo katika Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ambapo usaili huo unafanyika Mkoani Mbeya Katika Ukumbi wa Benjamini Mkapa uliopo Soko Matola Mkoani Mbeya.

Mpaka sasa Washiriki wapatao 150 wamejitokeza kwaajili ya kushiriki shindano hili la Tanzania Movie Talents ambapo washindi watatu kutoka kanda ya Nyanda za Juu Kusini watazawadiwa kitita cha Shilingi laki tano za Kitanzania na Baadae kupewa Tiketi ya Kuelekea Mkoani Dar Es Salaam kwaajili ya kushiriki fainali itakayowakutanisha Washindi waliopatikana katika Kanda ya Ziwa, Kati na kanda zilizobakia za Pwani na Kaskazini na mshindi katika fainali hiyo atajinyakulia Kitita Cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania pamoja na Mikataba minono kutoka Kampuni ya Proin Promotions Limited na washindi kumi katika fainali hizo watakuwa chini ya kampuni ya Proin Promotions Limited na kuweza kutengeneza filamu ya Pamoja ambapo watanufaika na Mauzo ya filamu yao.

Mashindano ya Tanzania Movie Talents yataendelea Mkoani Mbeya kwa Siku nne ambapo siku ya jumanne washindi wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini watapatikana na kupewa Zawadi zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...