Msanii Maarufu nchini Tanzania Mpoki a.k.a Muarabu wa Dubai ametua katika Jiji la Frankfurt na kuelekea moja kwa moja katika Jiji la Maraha Aschaffenburg ambapo atalala usiku mmoja na kuendelea na safari siku ya pili kuelekea Jiji La Berlin ambapo atahudhuria mkutano mkuu wa Umoja wa watanzania Ujerumani (U T U), Ngongamano la biashara pamoja na sherehe za muungano wa Tanzania.
Vyanzo vyetu vya habari vinanyetisha kwamba msanii huyo alitua katika uwanja wa kimataifa wa Frankfurt mnamo saa 10:30 alasiri na ndege ya shirika la ndege la Ethiopia Airlines akitokea Dar es salaam kupitia Addis Ababa. msanii huyo alipokelewa na mwenyekiti wa watanzania nchini ujerumani.
Tunawatakia watanzania wanaoishi ujerumani kila la heri na mafanikio katika sherehe hii kubwa na ya aina yake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...