Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdalah Kigoda na Balozi wa China Nchini Dkt. Lu Youqing wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa maonyesho ya siku nne ya bidhaa zinazotengenezwa nchini China.
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Shenzhen Yingli New Energy Resources Honglin Hui (Kulia) akimueleza Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdalah Kigoda (kushoto) jinsi Solar Panel inayotengenezwa na kampuni hiyo inavyofanya kazi wakati wa maonyesho ya bidhaa zinazotengenezwa nchini China yaliyofunguliwa leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee uliopo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdalah Kigoda akiangalia pikipiki aina ya SWAN inayotengenezwa na kampuni ya Honda ambayo inayotumia mafuta ya Petrol na Umeme wakati wa maonyesho ya bidhaa zinazotengenezwa nchini China. Kulia kwake ni Balozi wa China nchini Dkt. Lu Youqing na kushoto ni Juwes Wang ambaye ni mfanyakazi wa kampuni hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...