NANI kati wa washiriki 17 ataibuka kuwa mshindi wa shindano la Redd's Miss Temeke 2014, linalofanyika kesho kwenye Ukumbi wa TCC Club Chang'ombe Dar es Salaam.

Jumla ya warembo 17 kutoka vitongoji vya Mbagala, Kurasini na Chang;ombe watapanda jukwaani kuwania taji hilo, huku washindi wa tatu watapata nafasi ya kushiriki shindano la Miss Tanzania mwaka 2014.

Akizungumza Dar es Salaa jana Mkurugenzi BMP Promotions, Benny Kisaka, alisema kuwa maandalizi ya shindano hilo yamekamilika kama yalivyopangwa.

Kisaka alisema kuwa taji linaloshikiliwa na mrembo kutoka kanda ya kati, lakini mwaka huu Temeke imejizatiti kutoa si tu Miss Tanzania, mbali warembo watatu wa kwanza wa Taifa kutokana na viwango vya warembo wa mwaka huu.

Alisema kuwa mbali ya shindano hilo kubwa, kulifanyika shindano dogo la awali lililoandaliwa na Michuzi Media la Miss Photogenic ambalo mshindi wake atazawadiwa kitita cha Sh. milioni 1 taslimu, shindano ambalo lililsimamiwa na jopo la wapiga picha wa kampuni hiyo ambao watamtangaza na kumpa zawadi mshindi siku ya shindano.

Kisaka aliwataja Warembo wanaotarajiwa Subira Ally, Hellen Yughin, Catherine Alex, Dalina David, Winfrida Guntram, Salama Salehe, Grace John, Lilian Lothy, Amina Salim, Rebecca Mdamu, Sitti Mtemvu, Hellen Sule, Neema Mollel, Lucy Lewis, Esther Mnahi, Pauline Nkini na Patricia Ponsian ambao walikuwa chini ya ukufunzi wa Super Bokilo, Shadya Mohamed na Sweet Remmy.

Alisema mkali wa bongofleva, Khalid Mohamed TID almaarufu kama Top in Dar, sanjari na Wanne Star, Makirikiri wa Tanzania, Young Suma, Super Bokilo na wasanii mbalimbali wanatarajia kupamba shoo hiyo ambayo Dj John Peter Pantelakis atalisindikiza.

Wadhamini wa shindano hilo ni TBL Kupitia Redds wamedhamini shindano hilo sanjari na kinywaji cha Zanzi, Michuzi Media Group, Radio EFM 93.7 Cash & Carry Distributors, Kitwe General Traders, Rio Gym & Spa, CXC Africa, 88. 5 Clouds FM, City Sports Lounge, Gazeti la Jambo Leo, Kiwango Security na 100.5 Times FM.

BMP Promotions imeshakamilisha shindano hili la 19 tangu kuanzishwa Miss Temeke chini ya undaaji wake kwa asilimia kubwa, hivyo washabiki wa Kanda ya Temeke na vitongoji vyake watarajie mabadiliko makubwa katika aina ya shindano la urembo litakavyokuwa Ijumaa.

1996- Asela Magaka
1997- Miriam Odemba
1998- Khamisa Ahmed (Miss Temeke anayeendea kujiita hivyo huko Marekani)
1999- Ediltruda Kalikawe
2000- Irene Kiwia
2001- Happyness Sosthnes Magesse
super model Millen( Miss Tanzania)
2002- Regina Mosha
2003- Hawa Ismail ( Sylvia Bahame first runner up and Miss Tanzania same year)
2004- Cecylia Assey ( mrs Agrey Marealle), first runner up Miss Tanzania
2005- Seba Aggrey
2006- Jokate Mwegelo (Miss Tanzania fisrt runner up), Irene Uwoya 1st runner Temeke & 3rd runner up Miss Tanzania
2007- Queen David ( Miss Tanzania second runner up)
2008- Angela Lubala (top five Miss Tanzania)
2009- Sia Ndaskoy (top five Miss Tanzania)
2010- Genevieve Mpangala ( Miss Tanzania)
2011- Husna Twalib
2012- Edda Sylvester
2013- Svetlana Nyameyo ( Latifa Mohamedsecond runner Temeke and first runner up Miss Tanzania)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...