BIBI. URSULA SABINUS KWEKA
 1944 - 2014.

Kwa niaba ya Familia ya Mzee Sabinus Kweka, napenda kutoa shukrani za dhati kwa matendo, majitoleo na upendo wenu usiku na mchana kwa ajili ya mama yetu Mpendwa URSULA KWEKA kuanzia ugonjwa hadi kifo chake ambacho kilitokea usiku wa kuamkia tarehe 30/07/2014 na kuzikwa tarehe 05/08/2015 kijijini kwake NARUMU,wilaya ya HAI,mkoa wa KILIMANJARO. 

Kwa kuwa siyo rahisi kumshukuru kila mmoja kipekee, tunaomba mpokee nyote shukrani hizi kwa moyo mkunjufu. Kweli tumeuona utukufu wa Mungu. Ila tutakuwa Wachoyo wa fadhila kama hatutashukuru watu au vikundi vifuatavyo:-

1. Uongozi wote wa Mkoa wa Kilimanjaro ukiongozwa na  Mkuu wa Mkoa,Mhe.L.GAMA kwa kuwa nasi siku ya Mazishi 

2. Madaktari na Wauguzi wote wa Hospital za Dr.Mohamed,Selian – Arusha,pamoja na Bugando Medical Centre alikofia marehemu kwa huduma zao za kuokoa maisha ya marehemu bila mafanikio.

3. Majirani wa zamani wa Capripoint na wakazi wote wa Calfonia Nyegezi alikokuwa akiishi Marehemu

4. Ndugu,Jamaa na Marafiki popote walipo hasa wanarumu wa Mwanza na Watanzania waishio Marekani kwa michango yao ya hali na mali pamoja na maombi

5. Vikundi mbalimbali vilivyosaidia kuomboleza msiba K.m Jumaki, Umamwa,Ukiki,Tupendane,wafanyakazi wa Benki kuu Mwanza,Kweka Law Chambers,Kituo cha Utafiti Selian,Kwaya ya Mt.Augustino ya Parokia ya Mkolani kwa mkesha siku zote za maombolezo.

6. Mwisho,wanavijiji wote wa NARUMU, Waombolezaji  wote toka sehemu mbalimbali za Nchi, Mapadri na Masista wote walioshiriki Ibada ya Mazishi…………………………………………………………….

RAHA YA MILELE UMPE Eee BWANA………………………………

“HERI KUIENDEA NYUMBA YA MATANGA, KULIKO KUIENDEA NYUMBA YA KARAMU KWA MAANA HUO NDIO MWISHO WA WANADAMU WOTE” MHUBIRI 7:2

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...