JAMII nchini imepewa wito wa kuacha kudharau taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya hali ya hewa nchini ili kupunguza uwezekano wa kutokea majanga makubwa.

Wito huo umetolewa leo na Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, wakati akifungua warsha ya siku mbili kwa wanahabari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Hali hewa nchini (TMA).

Bendera ametoa wito huo siku mbili kabla ya TMA kutoa utabili wake wa hali ya hewa wa msimu wa Oktoba mpaka Desemba mwaka huu. Bendera alisema kuwa TMA imekuwa mstari wa mbele kutoa taarifa za hali ya hewa pamoja na tahadhari zake lakini wananchi walio wengi wamekuwa wakidharau tahadhari zinazotolewa na Mamlaka hiyo.

“Kama wananchi watakuwa wakifanyia kazi tahadhari zinazotolewa na TMA, itasaidia kupunguza madhara yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa.., Serikali inapata tabu kuwasaidia wananchi yanapotokea majanga.., lakini ukiangalia kabla ya majanga kutokea TMA wanakuwa tayari wameshatoa tahadhari ila sisi wananchi tuzidharau taarifa zao” alisema Bendera.

Aidha, alisema kuwa majanga ya hasili ni ngumu kuyaepuka lakini kupitia tahadhari za TMA inawezekana kupunguza madhara ya majanga hayo.

Kwa upande wake, akimkaribisha Mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi wa TMA, Dkt Agness Kijazi, alisema kuwa Mamlaka yake inatambua umuhimu wa wanahabari katika kufikisha taarifa za hali ya hewa kwa wananchi na ndio sababu ya kuwapa elimu itakayosaidia kuwaelimisha wananchi juu ya taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na mamlaka hiyo.

Katika hatua nyingine, Mamlaka hiyo mjini hapa kesho inatarajia kutoa utabiri wake wa mvua kwa msimu huu wa kuanzia Oktoba mpaka Desemba.
 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Warsha ya siku mbili ya Waandishi wa Habari ilinayoendeshwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini kuhusu umuhimu wa huduma za hali ya hewa,ushirikishwaji na usambazaji wa taarifa za hali ya hewa kwa umma,inayofanyika kwenye hoteli ya Oasis mjini Morogoro.Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini,Dkt. Agness Kijazi na kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini,Dkt. Hamza Kabelwa.Picha zote na Othman Michuzi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini,Dkt. Agness Kijazi akisisitiza jambo wakati akijubu moja ya maswali yaliyoulizwa na waandishi wa habari wanaoshiriki kwenye Warsha ya siku mbili ya Wanahabari inayoendeshwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini,inayohusu umuhimu wa huduma za hali ya hewa,ushirikishwaji na usambazaji wa taarifa za hali ya hewa kwa umma.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari wanaoshiriki kwenye Warsha ya siku mbili ya Wanahabari inayoendeshwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini kuhusu  umuhimu wa huduma za hali ya hewa,ushirikishwaji na usambazaji wa taarifa za hali ya hewa kwa umma wakisikiliza kwa makini hotuba ya ufunguzi wa warsha hiyo iliyokuwa ikisomwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera.
  Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini,Dkt. Hamza Kabelwa akizungumza jambo wakati akichangia moja ya mada zinazoendelea kuwasilishwa kwenye warsha hiyo inayoendelea hivi sasa kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Oasis,Mkoani Morogoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...