Baadhi ya Wajumbe wanawake wa Bunge Maalum la Katiba
wakiimba kwa furaha wakati wa semina iliyofanyika 30 Agosti, 2014
kwenye Ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba (wa kwanza kulia)
akipitia taarifa ya mapendekezo ya mtandao wa wanawake na Katiba
Tanzania wakati wa semina iliyofanyika 30 Agosti, 2014 kwenye
Ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma.
Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Bi. Usu Mallya akitoa
mada kuhusiana na suala la kijinsia katika Katiba, wakati wa Semina
iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa
Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu
masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye
Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
(Picha zote na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma).
Katiba yenye Mrengo wa Jinsia?? Hii yote ni siasa tu! Ukishajali haki za binadamu ndani ya katiba na ukaifanyia kazi, huna haja ya kuwa na mambo mengine, eti haki ya wanawake, watoto, walemavu, n.k.
ReplyDeleteUkiheshimu haki za binadamu bila kujali jinsia, rangi, elimu, umri, kabila, utakuwa umepunguza utitili wa makundi yanayoongeza gharama za uendeshaji wakati kunakuwa hakuna tija!!
Cha msingi ni kuondoa vichwani mwetu kitu kinaitwa "mfumo dume" tu! Mfume dume umeiua hii Dunia yetu, kwenye ngazi zote. Na kwa undani wanaume bado tunaogopa nguvu ya wanawake siku wakiamka na kujitambua kuwa wana uwezo mkubwa kuliko wanavyochukuliwa!
Hata kwa baadhi ya dini kuna harakati nyingi za kuwaacha nyuma wanawake kwenye majukumu mengi tu ya uongozi!
Ninachowaomba Wanawake wasije wakataka kulipiza, bali wautumie huo uwezo wao kwa kile kilichokusudiwa - maisha bora kwa kila kiumbe duniani!!
Wanaume???? Jiandaeni kwa mabadiliko!!
mujwahuki
kashonge.com