Kaimu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUba), Michael Kadinde (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam, kuhusu Tamasha la 33 la taasisi hiyo litakalofanyika kuanzia Septemba 22 hadi 28 mwaka huu. Kulia ni Mwenyekiti wa Tamasha hilo, Abraham Fadhil na Mkuu wa Mafunzo, Gabriel Kiiza.
Dotto Mwaibale

TAASISI ya sanaa na utamaduni Bagamoyo (TaSUba) imeanadaa tamasha la 33  lenye lengo la kukuza mila na desturi za watanzania.

Katika tamasha hilo kauli mbiu itakuwa sanaa na utamaduni katika kukuza utalii na mgeni rasmi ni Mbunge wa Afrika Mashariki Makongoro Nyerere ambaye atamwakilisha Spika wa Bunge la Afrika Mashariki, Spika wa Bunge hilo Margareth Zziwa .

Akizungumza  Dar es Salaam, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUba), Michael Kadinde alisema tamasha hilo pia lina lengo la kuonyesha sanaa zilizoandaliwa kiutalaam na wanafunzi wa Tasuba.

"Katika tamasha hili pia tuaihamasisha jamii ije ione tofauti ya sanaa iliondaliwa kitaalamu na isiyo kitaalamu kuweka ushindani kati kati ya taasisi yetu na vikundi vingine,"alisema.

Kadinde alisema katika taasisi yao wanafundisha maigizo,ngoma muziki ufundi wa majukwaa,sanaaza ufundina filamu za televisheni.

"Vikundi ambvyo vitashiriki katika tamasha hilo vya ndani ni 143 na vikundi vya nje vitakuwa vitano Kenya watakuwa na fani ya ngoma,Newzealand watakuwa na muziki, Norway, watakuwa na muziki,Newzealand muziki,Ujerumani maigizo na ,na Korea Kusini watakuwa na muziki,"alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...