Na Dotto Mwaibale

SERIKALI imesema itaainisha ukomo wa tozo kwa kila huduma inayotolewa kwa kila ngazi ya kituo cha huduma ili kudhibiti gharama za huduma za afya nchini.

Kauli hiyo ilitolewa  na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid Dar es Salaam leo asubuhi wakati akizindua bodi mpya ya ushauri ya Hospitali binafsi nchini.

Dk. Rashid alisema hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa malalamiko kuhusu huduma zinazotolewa na hospitali hizo hivyo hatua hiyo itasaidia kuboresha mfumo na kuwatendea haki wananchi wanaotumia vituo  vya kutolea huduma za afya.

"Malalamiko haya ni pamoja na huduma zisizo na ubora unaotakiwa na gharama zinazotolewa kwa huduma hizo .Sheria iliyopo inatutaka kudhibiti bei ya huduma hizi kwa kuzingatia malalamiko haya pamoja na matakwa ya sheria yenyewe," alisema Dk. Rashid.

Hata hivyo alibainisha kuwa licha ya kuwepo wa changamoto hizo huduma zinazotolewa na hospitali za watu binafsi zimechangia katika mafanikio  yaliyopatikana katika kufikia malengo ya maendeleo ya milenia.

Kuhusu bodi hiyo Dk .Rashid aliwataka wajumbe wapya wa bodi hiyo kufanya vikao vya mara kwa mara vinavyolenga uboreshwaji wa utoaji wa huduma.Na kuwataka kuendeleza utaratibu wa kusajili vituo vipya na kufupisha usajili kwa kutmia muda mfupi  kwa kutumia mfumo wa kielektroniki.

Alibainisha kuwa wajumbe wa bodi ya awali iliyosimamiwa na Mwenyekiti Dk. Deo Mtasiwa imesaidia kuboresha uwajibikaji wa wahusika hivyo kuboresha huduma na imeokoa maisha ya wananchi wengi ambayo yangekuwa hatarini endapo bodi isingetekeleza majukumu yake ipasavyo.

Alitaja wajumbe wa bodi mpya kuwa ni Dk.Donan Mbando ambaye ni Mwenyekiti, Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa mbeya Dk. Mpoki Ulisubisya, Mkurugenzi wa Hospitali ya Bugando Profesa Chalres Majinge, Mkurugenzi wa Tiba na Masuala ya Kiufundi (NHIF), DK. Frank Lekey.


Wajumbe wengine ni Mkurugenzi Msaidizi- Hospitali za Umma na Binafsi Idara ya Tiba Dk. Sijenunu Aaron, Mkurugenzi wa Association of Private Health Facilities (APHTA), Mwakilishi wa Mkurugenzi, Christian Social Services Comission (CSSC), Dk.Jane Kahabi na Mwanasheria Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Onorious Njole.
 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid, akizungumza na wajumbe wa bodi hiyo iliyomaliza muda wake na mpya wakati akizindua bodi hiyo Dar es Salaam leo asubuhi.
 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid (kulia),akimkabidhi cheti cha utumishi wa bodi hiyo,Profesa Bakari Lembariti. Katikati ni Mganga Mkuu wa Serikali, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Dk.Donan Mmbando. Vyeti hiyo walitunukiwa wajumbe wote waliomaliza muda wao.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...