Na Sultani Kipingo
Mtanganzaji mahiri nchini Gadner G. Habash amejiunga na kituo cha redio kinachiokuja kasi sana nchini cha EFM 93.7, Globu ya Jamii inaweza kuthibitisha. 
Gadner, ambaye alikuwa akipiga jalamba katika kituo cha Time FM baada ya kuondoka Clouds FM, pia hupasha-pasha mambo katika Michuzi TV, kwenye makala zake za kusisimua za "NAJUA WAJUA". 
"Ni kweli kaka. Sikiliza mambo kuanzia Jumatatu saa 9 alasiri hadi usiku. Kipindi kitaitwa 'Ubaoni". Gadner kaiambia Globu ya Jamii mchana huu. 
Gadner anakuwa mtangazaji mahiri wa pili kuhamia EFM, baada ya Maulid Baraka wa Kitenge kujiunga nao hivi karibuni akitokea Radio One Stereo. 
Globu ya Jamii inamtakia kila la heri Gadner G, Habash kwa kibarua hicho kipya ambacho hatuna shaka atakitendea haki kama ilivyo kawaida yake.


Pichani ni Gadner G. Habash (kulia) na Maulid Baraka wa kitenge wakiwa na Da'Mboni wa The Mboni Show TV talk show  wakijiandaa kurekodi kipindi kitachorushwa hivi karibuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...