CHAMA cha Waandishi wa Habari za Kodi Tanzania (TAWNET) umeipongeza kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania kwa kuwa moja kati ya walipa kodi bora wakubwa wa pili kwa mwaka 2014.

Sambamba na kampuni ya Vodacom, TAWNET pia imeipongeza kampuni ya bia Tanzania (TBL) na Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) kuweza kushika nafasi katika makampuni matatu bora. Mwaka huu, mchango wa Vodacom katika pato la taifa umeongezeka na kuisukuma kampuni hiyo katika nafasi ya pili kutoka ya tatu waliyoshika mwaka jana. 

Mkurugenzi Mtendaji wa TAWNET Judica Tarimo aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa, Vodacom imeshika nafasi ya pili bora kwa mara ya kwanza haijawahi kutokea na 
Kodi ni chanzo kikuu cha mapata kwa serikali na ndiyo inaiwezesha kutoa huduma kwa wananchi. Kwa niaba ya wana TAWNET napenda kutoa pongezi za dhati kwa Vodacom kwa kulipa kodi kwa uaminifu na pia makampuni mengine yafuate mfano huu, alisema.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa, Vodacom imekuwa mdau mzuri wa maendeleo kwa Watanzania na kuongeza kuwa uwekezaji wake umekuwa wa manufaa makubwa kwa nchi kwani pamoja na kuwa mlipa kodi mzuri wa pili, pia kupitia mfuko wake wa jamii kusaidia wa Vodacom Foundation kampuni hiyo imeweza kusaidia watanzania wenye matizo mbali mbali

Alisisitiza kuwa nchi inaweza kuondokana na utegemezi wa ufadhili endapo kila mtu na makampuni yatalipa kodi kwa uaminifu na kuzitaka mamlaka zinazohusika kuwa macho dhini ya watu na makampuni yanayotumia mbinu mbali mbali kukwepa kulipa kodi ahalali za serikali

Kuhusu kodi zilizolipwana Vodacom katika kipindi cha miaka miwili na kuifanya kampuni hiyo kuwa miongozi mwa walipa kodi bora Mtendaji wake Mkuu, Mkuu Rene Meza anasema“katika kipindi cha miezi sita cha mwaka wetu wa fedha kuanzia mwezi Aprili mpaka Septemba 2014,tumelipa kodi serikalini shilingi 27.6 bilioni/- kwa Kodi ya mapato,na tulikusanya shilingi bilioni 141.5 kwa kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na kodi ya zuio kwa niaba ya serikali”.

Pia aliongeza kuwa mwaka jana Vodacom ililipa kodi ya shilingi 47.1 bilioni/-kwa kodi ya mapato pia ilikusanya zaidi ya shilingi bilioni 262.8 za kodi ya Ongezeko la Thamani(VAT) ,kodi ya zuio na kodi nyinginezo zinazolipa serikalini. “Tunatimiza taratibu za kulipa  kodi kulingana na sheria za serikali na kuendelea kutimiza matakwa ya serikali.Ushindi huu tulioupata kwa mara ya pili ni uthibitisho wa kutosha”.Alisema.

Kuhusiana na uwekezaji mtendaji huyo Mkuu wa Vodacom anasema kampuni   hadi kufikia sasa Vodacom imewekeza nchini zaidi ya shilingi trioni 1.7/- na bado ina dhamira ya kuendelea kuwekeza na kukuza sekta ya mawasiliano nchini.

TAWNET ni asasi isiyokuwa ya Kiserikali inayojitegemea ambayo inaundwa na waandishi wa habari wenye mapenzi ya kuandika habari za kodi ikilenga kuwajengea  uwezo waandishi wa habari ili kubobea katika uandishi wa masuala ya kodi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...