Na Editha Karlo wa Globu ya Jamii, Kigoma 
 MKUU Wa Wilaya ya Kigoma Mhe  Ramadhani Maneno amewataka wananchi wa Wilaya ya Kigoma kuacha kuwashutumu viongozi wa wilaya na Halmashauri kuwa wamekula pesa za TASAF shilingi milioni 183,539 zilizotolewa na serekali kwaajili ya kusaidia kaya maskini Wilayani humo. 
Mhe  Maneno amewaambia wanahabari ofisini kwake leo kuwa pesa iliyotolewa na TASAF kwa ajili ya kusaidia kaya maskini na zinazoishi katika mazingira magumu katika Wilaya ya Kigoma zilikuwa pesa za mitaa 39. 
"Mpaka sasa katika mitaa hiyo 39 wamefanikiwa kulipa mitaa 36 na bado mitaa 3 ambayo ilikuwa na dosari katika taarifa zake za uhakiki ndo maana zoezi la kulipa mitaa hiyo ilisimama kwanza na pesa zao zipo salama katika akaunti ya Halmashauri.
"Mpaka sasa kuna fikra tofauti kwa baadhi ya wananchi kuwa kuna baadhi ya viongozi wa serekali wa Wilaya ya Kigoma wamekula fedha hizo za mitaa hiyo mitatu.
 ''Kwa kweli mimi ninachosema hizo pesa milioni 183,539 hakuna mtu yeyote aliyekula zipo katika mikono salama kwenye akaunti ya Halmashauri na taratibu zitakapo kamilika zitalipwa kwenye hiyo mitaa mitatu ambayo bado haijalipwa''alisema 
Mkuu huyo wa wilaya  alisema kuwa watumishi wa umma wote waliojiandikisha katika zoezi hilo na kusababisha mkanganyiko katika zoezi hilo watachukuliwa hatua za kinidhamu za kisheria za utumishi wa umma 
 Naye Mkurugenzi wa uratibu wa TASAF kutoka makao makuu Bw. Alphone Kyariga alisema kuwa TASAF awamu ya tatu imetoa msaada wa fedha kwa kaya maskini Wilaya ya Kigoma jumla ya shilingi milioni 249,822,000 kwa mitaa 39 ambayo inakadiliwa kuwa na kaya maskini 18,738. Alisema kuwa pesa zinazosemwa kuwa zimeliwa na viongozi milioni 183,539 zilikuwa ni pesa zilizotakiwa kulipwa katika mitaa mitatu nayo ni Burega,Sokoine na Lake Tanganyika lakini ilishindikana kuzilipa kwasababu ya mapungufu yaliyojitokeza katika mitaa hiyo. 
Bw.  Kyariga alisema kuwa zoezi la uhakiki wa kaya maskini katika mitaa hiyo ambayo haijalipwa zoezi la uhakiki na uandikishwaji litafnyika upya na wale wanaostahili kulipwa fedha hizo watalipwa kwani fedha zipo.
 ''Walio kuwa wakipita na kuandikisha kaya maskini ndiyo ili ziweze kusaidiwa na fedha za TASAF ndiyo walioleta mkanganyiko huu na kusababisha mitaa hiyo mitatu kushindwa kulipwa kwa wakati na kuonekana dosari mbalimbali ikiwemo kuandikisha watu wasio maskini kama vile watumishi, kaya moja kuandikishwa zaidi ya mara moja''alisema Mkurugenzi huyo.
  Alisema lengo la TASAF kutoa msaada huo ni kuwasaidia watu wenye kipato cha chini kabisa lakini kuna baadhi ya wananchi wenye uwezo wa kujikimu na maisha wanatumia fursa hiyo kujipenyeza ili na wao wapate msaada na kufanya viongozi kushindwa kukamilisha zoezi hilo ipasavyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake (ambao hawapo pichani) kuhusu taarifa zilizoeenea kuwa viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma wamekula hela za TASAF awamu ya tatu shilingi milioni 183,539,kushoto kwake ni Mkurugenzi wa utaribu kutoka makao makuu ya TASAF Alphonce Kyaliga 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...