Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara(MB) akikagua timu za Vijana waliochini ya miaka 15 kutoka Kinondoni na Dodoma ambazo zilishiriki hatua ya fainali katika mashindano ya Copa Coca Cola mwishoni mwa wikiendi katika uwanja wa Krume jijini Dar es Salaam. Ambapa katika fainali hizo kwa upande wanaume toimu kutoka Dodoma iliibuka bingwa wa mashindano hayo kwa kuichapa Kinondoni jumla ya magoli 4 -0, wakati kwa upande wa wanawake Kinondoni ilinyakua ubingwa kuifunga Ilala kwa mikwaju ya penati 2 – 1 baada ya dakika tisni kumaliza kwa sare ya mbili mbili.
Mchezaji wa timu ya mpira wa miguu wanawake kutoka Kinondoni akifunga penati wakati wa fainali za Copa Coca Cola 2014 katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam mapema wikiendi hii, Kinondoni ilinyakua ubingwa kwa kuifunga Ilala mikwaju ya penati 2 – 1 baada ya dakika tisni kumaliza kwa sare ya mbili mbili.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) (wa tatu kutoka kushoto) akifurahia mara baada ya kukabidhi zawadi ya mchezaji bora wa kike katika mashindano ya Copa Coca Cola kwa Golikipa wa timu ya Kinondoni Zubeda Mohamed (15). Wakwanza kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa Coca Cola Bw. Godfrey Njowoka, Rais wa TFF Jamal Malinzi na nyuma ya waziri anayecheka ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Leonard Thadeo.
Wachezaji wa timu ya Dodoma wakifurahia baada ya kukabidhiwa zawadi zao za ubingwa wa michuano ya Copa Coca Cola baada ya kuibuka mabingwa wa mashindano hayo kwa mwaka 2014 kwa mashindano hayo kwa kuichapa Kinondoni jumla ya magoli 4 -0, wakati kwa upande wa wanawake Kinondoni ilinyakua ubingwa kuifunga Ilala kwa mikwaju ya penati 2 – 1 baada ya dakika tisni kumaliza kwa sare ya mbili mbili. Picha na Frank Shija, WHVUM.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...