Rais wa Kwanza wa Zambia Dkt.Kenneth Kaunda akimkaribisha nyumbani kwake Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete huko kijijini kwake Mkango Barracks, State Lodge nje ya jiji la Lusaka leo Dkt. Kaunda ambaye alimwalika Rais Kikwete alifanya naye mazungumzo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la mke wa Rais wa Kwanza wa Zambia Mama Betty Mutinkhe Kaunda huko Mkango Barracks,State lodge, nje ya jiji la Lusaka leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha wageni nyumbani kwa Rais wa Kwanza wa Zambia Dkt.Kenneth Kaunda(aliyesimama akiangalia) leo wakati alipomtembelea mwasisi wa taifa hilo

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Edgar Lungu wa Zambia wakigonga glasi wakati wa dhifa ya kitaifa aliyoiandaa kwa heshima ya Rais Kikwete jijini Lusaka Zambia jana jioni.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akigonga glasi na Rais wa Kwanza wa taifa la Zambia Dkt.Kenneth Kaunda wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais Kikwete jijini Lusaka Zambia jana jioni.Rais Kikwete ambaye alikuwa katika ziara ya siku mbili nchini Zambia tayari amerejea jijini Dar es Salaam.

Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais wa Zambia Edgar Lungu pamoja na wake zao Mama Salma Kikwete na Mama Esther Lungu wakinyanyua glasi juu wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais Kikwete na ujumbe wake ambao walifanya ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Zambia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongera JK kwa kuwakumbuka wazee waliopigania nchi hii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...