Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu akizungumza na katika mkutano uliohusisha wadau wa mashirika ya Kimataifa na asasi za kijamii ukiwa na lengo la ushirikishaji wa jamii katika masuala ya uhifadhi wa wanyamapori uliofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa Mpingo House uliopo Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Maliaisli na Utalii, Mahmoud Mgimwa akitoa salamu kwa wadau wa taasisi za kirai. Kushoto Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu.
Mratibu wa Uhakiki wa Ubora kutoka Haki Elimu, Robert Mihayo akitoa maoni kwa Waziri Mh. Nyalandu ambapo amemuomba kushirikisha wadau wa elimu katika kutoa elimu ya uhifadhi wa wanyamapori kuanzia ngazi ya elimu ya msingi ili kuwaanda vijana ambao ni taifa la kesho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...