Na Editha Karlo wa Globu ya Jamii, Kigoma 
 MKUU wa wilaya Uvinza Hadija Nyembo ameitaka jamii kujitokeza kwa wingi kupeleka watoto wao kupatiwa chanjo ya kujikinga na magonjwa mbalimbali na kuachana na imani potofu kwamba chanjo zimeletwa kwa madhumuni tofauti ikiwemo kudhibiti suala la wanawake wasizae watoto wengi. 
 Akizundua siku ya chanjo kitaifa kwa wilaya ya Uvinza Mkuu wa wilaya hiyo,Hadija Nyembo amesema kuwa jamii inao wajibu mkubwa wa kuhakikisha inawapeleka watoto wao kupata chanjo huku akihimiza wanaume kujitokeza kwa wingi kuwasindikiza wake zao kliniki. 
 Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa chanjo za magonjwa ikiwemo kifaduro,pepo punda, polio na nyinginezo zimekuwa na faida kubwa kwa watoto na ndiyo maana serikali imekuwa ikitumia mbinu mbalimbali kuhakikisha jamii inapata chanjo hiyo. 
 Awali Afisa afya wa wilaya ya Uvinza,Rajabu Katole alisema kuwa jumla ya watoto 34,000 sawa na asilimia 96 ya watoto wanaoishi katika wilaya ya Uvinza wanatarajiwa kupatiwa chanjo mbalimbali katika maadhimisho hayo ya siku ya chanjo kitaifa wilayani humo. 
 Katole alisema kuwa pamoja na malengo hayo wamekuwa wakikabili na upungu mkubwa wa watumishi wa sekta ya afya na hasa watumishi wenye utaalam wa mambo ya chanjo jambo ambalo limewafanya wakati wa kuanza chanjo hizo kutoa maelekezo ya mara kwa mara kwa watumishi waliopo waweze kutekeleza jukumu la kufanikisha chanjo hizo. 
 Kwa upande wake Mganga Mkuu wa wilaya Uvinza, Albert Mumwi amesema kuwa watu wengi kuishi mbali na vituo vya utoaji huduma ya afya ni moja ya changamoto zinazowakabili wakati wa zoezi la kuendesha chanjo mbalimbali kwa watoto chini ya miaka mitano. 
 Mumwi alisema kuwa baadhi ya maeneo yako zaidi ya kilometa 40 kutoka kilipo kituo cha utoaji huduma katika sekta ya afya na hivyo kuwalazimu kuanzisha huduma ya Mkoba unaotembea na hivyo kuwafuata watu hao huko walipo wengi wao wakiwa ni wakulima.
 Mkuu wa wilaya ya Uvinza Hadija Nyembo (kushoto) akitoa matone ya chanjo ya polio kwa mmoja wa watoto waliohudhuria uzinduzi wa siku ya chanjo mbalimbali kwa watoto iliyofanyika kiwilaya kwenye mji mdogo wa Uvinza mkoani Kigoma.
Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Khadija Nyembo akisoma hotuba yake ya uzinduzi wa chanjo ya polio kwa wananchi Wilaya ya Uvinza waliohudhuria uzinduzi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...