KESI ya kugombea  mirathi ya mwandishi wa habari mkongwe nchini marehemu Betty Luzuka (pichani) imeibua mapya  mahakamani mara baada ya ushahidi wa njia ya video kumuonyesha mke wa aliyekuwa ofisa mwandamizi wa  jumuiya ya  Afrika Mashariki ,Phil Makini Kleruu aitwaye Hilda Kleruu akichukua fedha za marehemu kabla na baada ya marehemu kuaga dunia.

Hilda, ambaye amefunguliwa kesi na kaka wa marehemu, Ssarongo Luzuka akimtuhumu kujimilikisha mali za marehemu bila kufuata utaratibu wa kifamilia na kimahakama mara baada ya marehemu kuaga dunia Agosti mwaka 2013 katika hospitali ya Shreee Hindu ya jijini Arusha baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kesi hiyo ya mirathi inayovuta hisia za watu mbalimbali jijini Arusha  ipo katika mahakama ya mwanzo ya Maromboso  yenye nambari 222 ya mwaka 2013 inaitaka mahakama hiyo ipitie hukumu yake iliyotolewa Septemba 27 mwaka 2013  na hakimu Prince Gideon iliyompa  ushindi kaka wa marehemu. Kwa habari kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...