Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mhandisi
Edwin Amandus Ngonyani (pichani) kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa
(Stamico). Uteuzi huo umeanza Jumapili iliyopita, Juni 28, 2015.
Taarifa
ya kuthibitisha uteuzi huo iliyotolewa Ikulu, Dar es salaam na Katibu Mkuu Kiongozi
(KMK) leo, Jumanne, Juni 30, 2015, inasema kuwa kabla ya uteuzi wake Mhandisi Ngonyani alikuwa Mkaguzi Mkuu wa
Migodi na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Stamico.
Mhandisi
Edwin Ngonyani ni mhandisi wa migodini mwenye uzoefu wa muda mrefu wa sekta ya madini.
Anayo shahada ya kwanza ya fani hiyo kutoka Chuo Kikuu cha Zambia na shahada ya
uzamili (MSC) kwenye fani hiyo hiyo kutoka Chuo Kikuu cha Exeter, Camborne
School, Uingereza.
Mhandisi
Ngonyani amefanya kazi nzuri wakati anakaimu nafasi ya Ukurugenzi Mtendaji
na kwa kumteua, Rais Kikwete ana imani kubwa kuwa ataendeleza kazi hiyo nzuri ya
kuimarisha uwekezaji wa umma katika sekta hiyo ya madini kupitia Stamico.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
30 Juni, 2015
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...