Muonekano wa Banda la Mahakama ya Tanzania
likiwa katika Viwanja vya Julius Nyerere maarufu kama Viwanja vya Sabasaba,
Mahakama ya Tanzania inashiriki katika Maonesho haya lengo likiwa ni kutoa
fursa kwa wananchi kupata elimu juu ya taratibu mbalimbali za Mahakama ikiwa ni
pamoja na kutoa Malalamiko pamoja na kupokea maoni ya jinsi ya kuboresha huduma
ya utoaji haki nchini. Banda la Mahakama lipo mkabala na Banda la
Zanzibar ndani ya viwanja vya Sabasaba. Katika Maonesho ya mwaka huu, Mahakama ya Tanzania
imepanua wigo wa kutoa huduma zake ambapo katika banda hilo kuna uwakilishi wa
kila ngazi ya Mahakama kuanzia Mahakama za Mwanzo, Mahakama za Wilaya/Hakimu
Mkazi, Mahakama Kuu pamoja na Divisheni zake ikiwa ni Divisheni ya Ardhi,
Biashara na Kazi na Mahakama ya Rufani (T).
Vilevile katika banda hilo pia kuna elimu inatolewa
kuhusiana na taratibu mbalimbali za ufunguaji wa kesi za mirathi na kadhalika,
wananchi wote wanakaribishwa kutembelea banda hilo.
Bi. Wanyenda Kutta, Mkurugenzi Msaidizi wa
Utumishi, Mahakama akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yahusuyo Mahakama kwa
vijana wa scout waliotembelea banda hilo
Vijana wa scout wakipata maelezo kuhusu mahakama
Mhe. Eva Nkya, Naibu Msajili Mwandamizi,
Mahakama Kuu ya Tanzania akifafanua jambo kwa moja ya wateja waliotembelea
banda la Mahakama
Mhe. Frank Mahimbali, Naibu Msajili- Mahakama
Kuu Divisheni ya Ardhi akisisitiza jambo kwa wateja waliokuja kupata elimu ya
Mahakama.
Picha na Mary Gwera, Mahakama.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...