Rais Mstaafu Alhaj Dkt Ali Hassan Mwinyi alizuru Jamhuri ya Watu wa China kufuatia mualiko uliomhitaji ashiriki na kutoa hotuba katika ufunguzi wa mkutano wa kuadhimisha miaka sabini ya kuundwa kwa Umoja wa Mataifa tarehe 20 Julai 2015. 

Katika ziara hiyo, Rais Mwinyi pia alipata fursa ya kutembelea Ubalozi wetu na kupata chakula kilichoandaliwa na Balozi wa Tanzania nchini China, Jenerali (Mstaafu) AbdulRahman Shimbo pamoja na Mama Shimbo.
Rais Mstaafu Mwinyi, Mama Sitti Mwinyi na wadau wengine wakiwa ziarani Guangdong

Rais Mwinyi pia alipata fursa ya kuzuru maeneo mbalimbali jijini Beijing pamoja na Zhuhai na Guangzhou katika jimbo la Guangdong. Katika ziara hiyo, Mwinyi alikutana na viongozi waandamizi katika maeneo yote aliyotembelea katika ziara yake na pia alipata fursa ya kutembelea Mamlaka inayosimamia ujenzi wa daraja la Hongkong – Zhuhai – Macau miongoni mwa maeneo mengine. 

Daraja la Hongkong – Zhuahi – Macau litakuwa na urefu wa zaidi ya kilomita hamsini na linavuka bahari kuunganisha Bara ya China na visiwa vya HongKong na Macau halitokuwa kivutio tu, bali linaonesha umahiri wa watu wa China katika fani za ubunifu na uhandisi.
Rais Mstaafu Mwinyi akisaini kitabu cha wageni cha makumbusho ya mipango miji jijini Beijing.

Rais Mwinyi aliondoka China kurudi nyumbani usiku wa tarehe 26 mwezi Julai 2015 akiwa ameambatana na Mama Sitti Mwinyi. Ziara hii ya Rais Mwinyi ni ishara kuwa mataifa haya marafiki (China na Tanzania) yanaendelea kuuthamini urafiki wao usio wa msimu na kuwa uhusiano huo utadumishwa ili uwe urithi wa vizazi vijavyo na wao wauendeleze. 

Tanzania na China wana uhusiano wa miongo mingi ambapo China ilivutiwa na kujenga reli ya TAZARA – reli ya pekee iliyojengwa Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara katika kipindi cha miaka 50 iliyopita.

Imetolewa na Ofisi ya Rais Mstaafu Dkt Ali Hassan Mwinyi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...