Daktari wa Kwanza Bingwa Mshauri wa Maradhi ya Moyo kutoka Hospitali ya Rufaa ya Morogoro nchini Tanzania Dr.Harun Elmada Nyagori azawadiwa Tuzo ya Kimataifa na kutambuliwa na Baraza la Madaktari Bingwa wa shirikisho la Nchi za Ulaya(European Society of Cardiology) -London Uingereza'
Akipewa hiyo Tuzo ya Heshima na Rais wa Shirikisho Hilo Prof.Pinto alimwelezea imekuwa Historia kubwa kumpata Daktari aliyewakilisha Mada za Utafiti wa Maradhi ya Moyo kutoka Tanzania na hawajawahi kumpata Mtanzania aliyewahi kuingia kwenye Shirikisho Hilo 
Hivyo Dr Nyagori amefungua mlango kwa Madaktari wengine kufanya tafiti mbalimbali zinazohusu hiyo taaluma ya magonjwa ya Moyo.
Dr Nyagori akiwa na muasisi wa Kimataifa na Mwandishi wa Vitabu vikuu wa taaluma hiyo Prof.Eugine Brawnward 
 Dr Nyagori na Rais wa Shirikisho Hilo la Madaktari Bingwa wa Maradhi ya Moyo prof.Pinto Dr Nyagori amealikwa na Shirika la Utangazaji BBC kwa mdahalo maalumu kuhusu hiyo Tuzo,taarifa kamili zitarushwa Focus on Africa
Dr Nyagori akiwa na wajumbe wenza walioteuliwa kuingia kwenye Shirikisho Hilo la Madaktari Bingwa wa Ulaya wakiwa na Rais wa Shirikisho Hilo Prof.Pinto

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Hongera sana.

    ReplyDelete
  2. Hongera nyingi sana kwako daktari kwa kupata heshima hiyo iliyotukuka katika masuala ya utafiti wa maradhi ya Moyo yanayoikabili Tanzania.

    Mdau
    Christos Papachristou
    Diaspora

    ReplyDelete
  3. Not many of these in Bongoland. How on earth is he based in Morogoro and not at Muhimbili?

    Congrats to him and all the best.

    ReplyDelete
  4. Hongera sana Dr Harun, umeonyesha njia njema kwa vijana wa kitanzania.

    Tuwache kulalamika na kushabikia siasa tufanye kazi na sisi tupate kutambuliwa kimataifa.

    ReplyDelete
  5. Hongera daktari kwa kutambuliwa kimataifa kutokana na utafiti wako wa kiwango, tunakutakia mafanikio katika kufanikisha matibabu ya moyo kitaifa na kimataifa. Hongera sana.

    ReplyDelete
  6. Hongera sana Dr. Nyagori kwa kazi nzuri. Hivi Dr. Janabi alipataga tuzo au alipata utambuzi wa namna gani kimataifa? Nadhani sasa tuna madaktari wawili bingwa wanaotambuliwa kimataifa.

    Hongereni sana. Kwa mwenye kumbukumbu naomba anikumbushe recognition ya Dr. Janabi ilikuwa ya kitu gani nadhani miaka 3 au 4 imesihapita.

    Madaktari wengine endelezeni jitihada zenu. Nimekumbuka pia kuwa.Dr..Makani naye alitambuliwa Kimataifa. Hivyo watanzania tunasonga mbele kwenye fani ya utabibu.

    ReplyDelete
  7. Hongera sana Dr.Nyagori umetoa fundisho kwa watanzania. Mungu azidi kukuinua....we are proud of you.

    ReplyDelete
  8. Dokta umetisha yani hongera mnoo naamini watanzania watakua na chakujifunza kupitia wewe..BRAVO!! We are proud of you.

    ReplyDelete
  9. Hongera xana. Am happy for you

    ReplyDelete
  10. Hongera sana Dr. kwa kazi nzuri na kwa kulitangaza vizuri jina la nchi yetu.

    ReplyDelete
  11. Dr. Hongera mno mno kwahatuahyo uliyopiga kwani itafungua milango kwa madaktari wengine hapa Tanzania kushiri kwenye tafti mbalimbali duniani kote

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...