Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA
kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa
akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa
wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Sabasaba Gangilonga,
Mkoani Iringa, Agosti 30, 2015. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI, IRINGA.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA
kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa,
akiwahutubia maelfu ya wananchi wa Iringa Mjini waliofurika kwenye
Uwanja wa Sabasaba Gangilonga, Agosti 30, 2015. Katika Hotuba yake Mh. Lowassa
alizungumzia namna atakavyotoa kipaumbele kwa wakulima ambapo amesema
atafuta ushuru wa mazao kwa wakulima na kufuta kodi kwa vifaa vya
michezo na burudani ili vijana waweze kunufaika na vipaji vyao.
Umati
wa Wakazi wa Mji wa Iringa Mjini ukiwa umefurika kwa wingi kwenye
Uwanja wa Sabasaba Gangilonga, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa
Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, Agosti
30, 2015.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA
kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa
akimsalimia kijana mwenye ulemavu (jina lake hakupatikana kwa haraka)
aliyehudhulia Mkutano wa Kampeni ya Mgombea huyo, uliofanyika kwenye
Uwanja wa Sabasaba Gangilonga, Iringa Mjini, Agosti 30, 2015. Kushoto ni Waziri
Mkuu Mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye.
KUONA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA AU BOFYA HAPA
KUONA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA AU BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...