Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anna Makinda akiwa  katika Mkutano wa Kumi wa  Maspika  Wanawake uliofanyika kwa siku mbili  hapa  Umoja wa Mataifa, Mkutano wa Maspika Wanawake, umetangulia Mkutano wa Nne wa Maspika zaidi ya 180 unaoza leo jumatatu hapa Umoja wa Mataifa.
Sehemu ya  Wajumbe wa Mkutano wa Kumi wa Maspika  wanawake,   mkutano  uliojadili mbinu za kuchagiza  usawa wa kijinsia, miaka 20 baada ya Beijing pamoja na  kuhakikisha utekelezaji  wa malengo 17  ya Maendeleo Endelevu Baada ya 2015.
  Maspika  Wanawake wakiwa  katika picha ya pamoja  na Rais wa IPU Bw.  Choedhury Saber na  Katibu Mkuu wa IPU Bw. Martin Chungong wakati wa mkutano wao wa siku mbili uliofanyika  jumamosi na jumapili, ukitangulia  mkutano wa nne wa Maspika  wa  Mabunge.


Na Mwandishi Maalum, New York
MKUTANO wa Nne  unaowakutanisha Maspika  180 na Manaibu Spika 35 kutoka nchi 140,  unaanza leo ( jumatatu) hapa Makao Mkuu ya Umoja wa Mataifa.

Mkutano  huu wa siku tatu na  ambao umeandaliwa  na  Chama cha Mabunge Duniani ( IPU), utafunguliwa na Rais wa  IPU  Bw. Chowdhury Saber na Katibu Mkuu wa Umoja wa Matafa,  Ban Ki Moon.

Spika wa Bunge  la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Ann Makinda  anaongoza  ujumbe wa Tanzania katika mkutano huu.

 Mkutano ambao  Maspika wanatarajiwa kujadiliana kwa kina namna ya kukabiliana na changamoto za Amani, Demokrasia na Maendeleo kwa  maono ya Kibunge.

Mkutano wa Nne wa Maspika,  ulitanguliwa na   Mkutano wa Kumi   wa  Maspika wanawake,  mkutano  uliofanyika kwa siku mbili ( jumamosi na Jumapili). Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Ann Makinda ameshiriki kikamilifu na  kuongoza baadhi ya  mikutano.

Mkutano wa  Nne wa Maspika ni sehemu ya  mfululizo wa mikutano ya Maspika hao  na ambayo imekuwa  ikifanyika kuelekea Mkutano wa Kilele wa Viongozi wakuu wa Nchi na Serikali utakaofanyika wiki chache zijazo ambapo watapokea na kupitisha  Ajenda Mpya za  Maendeleo Endelevu  baada ya 2015.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...