Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florens Turuka (mwenye miwani) akimsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, Patrick Karangwa wakati alipokagua ujenzi wa nyumba za waathirika wa maafa Kijijini Mwakata, Kahama, tarehe 30 Agosti, 2015.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florens Turuka akimsikiliza mwenyekiti Kijiji cha Mwakata wilayani Kahama, Ezekieli Ramadhani akitafsiri kwa Kiswahili shukrani zizokuwa zikitolewa kwa kisukuma na Bi. Rugumba Msenga kwa serikali kumjengea nyumba kutokana na nyumba yake ya awali kuathirika na maafa ya Mvua, wakati Katibu Mkuu huyo alipokagua ujenzi wa nyumba za waathirika hao zilizojengwa na SUMA JKT, tarehe 30 Agosti, 2015.
Muonekano wa nyumba mpya ya muathirika wa maafa ya mvua kijijini Mwakata Kahama. Rugumba Msega (hayupo pichani ) ambayo amejengewa na serikali kupitia Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa usimamizi wa SUMA JKT, kulia ni makazi ya muda aliyokuwa amejengewa na serikali na mbele ya nyumba hiyo ni mabaki ya nyumba yake ya awali iliyoathirika na maafa hayo, tarehe 30 Agosti, 2015.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florens Turuka akiagana na mwenyekiti Kijiji cha Mwakata wilayani Kahama, Ezekieli Ramadhani mara baada ya kukagua ujenzi wa nyumba za waathirika wa maafa ya mvua zilizojengwa na SUMA JKT, tarehe 30 Agosti, 2015, kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji SUMA JKT, Kanali Felix Samillan na Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Gen, Mbazi Msuya (mwenye kofia ).
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florens Turuka (mwenye miwani) na Mkuu wa Wilaya ya Kahama ( kulia kwake), Benson Mpesya wakiwa katika picha ya pamoja na waratibu wa shughuli za maafa Mwakata kutoka; Ofisi ya Waziri Mkuu, SUMA JKT, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Shinyanga, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kahama na Halmashauri ya Msalala mara baada ya kikao cha ujenzi wa nyumba za waathirika wa maafa ya mvua Mwakata, tarehe 30 Agosti, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kutumia jeshi hata magereza wakati huu wa amani kuboresha makazi ya wananchi kuendelee siyo tu kwa wenye maafa na walioathirika na mabomu bali hata watanzania wengine wenye mazingira magumu ya kuishi. Hata balozi mmoja wa nje alitoa hoja hii ya msingi inayoweza kuharakisha maendeleo na kuboresha hali za maisha juzi juzi. Viongozi waendeleze miradi hii ya maendeleo katika jamii zenye nyumba duni kama kwa mfano za baadhi ya wabarbaig wenye nyumba duni, baadhi ya jamii zinazopokea misaaada ya TASAF za karatu kwa mfano zina nyumba duni sana, moja ya nyumba zao za kienyeji ziwe makumbusho, wao wawezeshwe kwa mtindo huu kuboreshewa maisha wakifuatiwa na jamii nyingine maskini wakitegewa pia maji ya mvua na kuwezeshwa kuwa na nishati ya biogas ya kupikia na sola ya kuwasha. Kuziacha baadhi ya jamii hizi bila msaada hazitabadilika karibuni. Kila mkoa uwe na mikakati kama hii ili kuharakisha maendeleo ya watanzania na kuondoa ufukura.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...