Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Ismail Juma(kushoto) akikabidhi jezi kwa kapteni wa timu ya G Unity Fc kwa ajili ya mchezo wa fainali uliofanyika katika kiwanja cha Kipunguni B katika kata ya Kipunguni manispaa ya Ilala jijini Dar. Ambapo timu ya G Unity FC waliibuka washindi baada ya kuichapa timu ya Sukuma Land Fc bao 5 kwa 2.
Mmoja wa Madereva Bodaboda akisoma maelekezo ya jinsi ya kutuma pesa kwenye akaunti kwenye mfuko wa Uchangiaji wa Hiari(PSS) mara baada ya kupatiwa kitambulisho cha uanachama wa mfuko wa PSPF.
Maafisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF wakiwa kwenye picha ya pamoja na waratibu wa michezo hiyo pamoja na Timu ya G Unity Fc walioibuka washindi wa wa kwanza baada ya kufunga timu ya Sukuma Land Fc mabao 5 -2, mchezo huo uliofanyika katika kiwanja cha Kipunguni B
Mbwembwe za mashabiki katika fainali hizo
Mkurugenzi mtendaji wa kata
ya Kipunguni na Kivule Dr. Kadry Pinde ambaye alikuwa ni Mgeni rasmi katika mchezo wa
fainali akikabidhi mpira kwa kapteni wa timu ya Kilimani Fc walioibuka washindi
wa wa nne katika mashindano ya mpira wa miguu kwa madereva Bodaboda wa kata ya
Kipunguni. Wa kwanza kushoto ni Afisa
Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Ismail Juma.
Mashabiki wakiendelea kufuatia kinachijili uwanjani
MASHINDANO ya ligi wa mpira wa
miguu kwa madereva bodaboda yahitimishwa na wadhamini wa mashindano hayo ambao
ni mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa kuweza kuwasajiri wachezaji katoka mfuko wa
hiari wa PSS. Ligi hiyo iliyodumu ndani ya siku saba (7) ambapo alikuwa
akitafutwa mshindi atakayeweza kuwa balozi mzuri wa mfuko wa penshenI wa PSPF
yamemalizika kwa timu 32 kumenyana vikali na timu ya G Unity kuibuka
kinara ambapo timu hiyo ndiyo iliyotawazwa na kuwa balozi wa PSPF katika kata
ya Kipunguni mara baada ya fainali iliyohusisha timu ya Sukuma Land FC na
G Unity Fc na hatimaye timu yaG Unity kuibuka kinara kwa bao 5 kwa2 katika
fainali iliyopigwa katika kiwanja cha Kipunguni B.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...