Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
BAJETI ya Manispaa ya Ilala kwa mwaka wa fedha 2015/2016 ni sh.bilioni 55 kutoka sh.bilioni 30 ya mwaka wa fedha 2014/2016. 

 Akizungumza katika baraza la madiwani katibu wa baraza hilo na Mkurgenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mngurumi (Pichani)  amesema kuwa kutokana na bajeti hiyo kuwa juu madiwani wanatakiwa kufanya kazi katika kubuni vyanzo vya mapato. 
 Amesema kuwa baraza ndilo linaweza kufanya bajeti hiyo ikatimia katika makusanyo kutokana na vyanzo vya mapato vilivyopo au kuongeza vyanzo vingine. Mngurumi amesema katika kuanza kufanya kazi kwa baraza la madiwani lazima kamati zipatikane ambapo hilo limefanyika kwa kufanya uchaguzi. 
 Aidha amesema kuendana na bajeti hizo kamati ziweze kujadili bajeti jinsi ya kuweza kupata bajeti itakayosaidia kuendesha na kutoa huduma kwa wananchi wa manispaa ya Ilala. Meya wa Manispa kwa ya Ilala, Charles Kuyeko amewataka madiwani kujadili kwa kina bajeti hiyo katika kamati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...