HOTUBA YA MHE. KASSIM MAJALIWA MAJALIWA (MB), WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WAKATI WA KUHITIMISHA SHUGHULI ZA MKUTANO WA PILI WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAREHE 5 FEBRUARI, 2016

I:       UTANGULIZI
(a)                Masuala ya Jumla

Mheshimiwa Naibu Spika,
1.            Kwanza nianze kwa kumshukuru Mungu kwa kutujalia afya njema na uwezo katika kutenda yote yaliyo mema. Tumekuwepo hapa kwa takriban siku 11 katika shughuli za Mkutano wa Pili wa Bunge lako Tukufu. Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa Rehema kwa kutufikisha salama siku ya leo.

2.            Tumekutana hapa tukiwa tumeshuhudia uundwaji wa Serikali unaoendelea ambapo Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya uteuzi wa Baraza jipya la Mawaziri ambao ni Waheshimiwa Wabunge wenzetu. Niruhusu nitumie nafasi hii ya awali kuwapongeza Mawaziri na Naibu Mawaziri wote ambao wameteuliwa kushika nyadhifa mbalimbali katika Serikali ya Awamu ya Tano.

(b)        Chaguzi Mbalimbali  

Mheshimiwa Naibu Spika,
3.            Katika Mkutano huu, tumeweza kufanya Chaguzi za Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge. Vilevile, tumefanya chaguzi za Wenyeviti wa Bunge letu na Wajumbe wa kutuwakilisha katika Taasisi mbalimbali za Kitaifa na Kimataifa. Kwa vile orodha ni ndefu, napenda nitumie nafasi hii kuwapongeza kwa dhati kabisa na kwa ujumla wao wote waliogombea nafasi hizo na kushinda. Ni matarajio yangu kwamba tutatumia nafasi hizo vizuri katika kuleta ushirikiano, mshikamano na kufanya kazi pamoja kama Wawakilishi wa Wananchi na kutekeleza majukumu yetu kama Wabunge ndani ya Bunge hili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...