Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakishiriki kupanda mihogo kwenye shamba ya la Wahadzabe kwenye kijiji cha Kibampa wilaya ya Mkalama.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Ndugu Christopher Ngubiagai akimuelekeza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana namna Wahadzabe wanavyosaga mtama kwa kutumia jiwe.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana leo ameweka historia ya kuwa kiongozi wa nne mkubwa wa Kitaifa kufika kwenye kijiji cha Munguli na Kibampa ambavyo wanaishi jamii ya Wahadzabe .Kijiji cha Munguli kilitembelewa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kamabarage Nyerere, akifuatiwa na aliyekuwa Makamu wake Abdu Jumbe na Mama Sofia Kawawa.
Jamii ya Wahadzabe inaishi kwa kutegemea uwindaji,kula matunda ya porini,mizizi ,wadudu na miti hata hivyo juhudi kubwa zimefanyika kuanza kuwafundisha kilimo, kuwapeleka watoto shule ,zaidi ya Wahadzabe 305 wanasoma kwenye shule ya msingi Munguli, pamoja na vijana zaidi ya 50 kupelekwa kujiunga na JKT.
Katika ziara hiyo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone kwa jitihada zake za kuwasaidia jamii ya Wahadzabe ikiwa pamoja na kuhakikisha wanapata elimu, wanajifunza kilimo lakini pia uamuzi wa kupima maeneo ya Wahadzabe ili wamiliki ardhi yao wenyewe.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) akiwa kwenye nyumba maalum ya chifu wa wahadzabe pamoja na Mwenyekiti wa Wahadzabe Edward Mashimba na Mama Sarah Philipo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoka kwenye nyumba ya Chifu wa Wahadzabe iliyopo kijiji cha Kibampa kata ya Mwangeza wilaya ya Mkalama mkoani Singida.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha
Kibampa ambako wakazi wake ni jamii ndogo yenye kaya 300 ya
Wahadzabe,kushoto ni Mwenyekiti wa Wahadzabe Ndugu Edward Mashimba
(kushoto) ambaye alikuwa akitafsiri kwa lugha ya Kihadzabe.
wakazi wa kijiji cha Kibampa ambako wakazi wake ni jamii ndogo yenye kaya 300 ya Wahadzabe wakishangilia jambo wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Kibampa ambako wakazi wake ni jamii ndogo yenye kaya 300 ya Wahadzabe,kushoto ni Mwenyekiti wa Wahadzabe Ndugu Edward Mashimba (kushoto) ambaye alikuwa akitafsiri kwa lugha ya Kihadzabe
Hilo jiwe la kusagia mtama (nafaka kwa jumla) binafsi limenikumbusha mbali sana, enzi hizo bibi zetu (Mwenyeez Mungu awarehem huko waliko - Amen) nakumbuka walikuwa wakisagia nafaka mbali mbali mpaka majani makavu ya mrenda, huku wakiimba nyimbo zao za kiasili ili kuji 'motivate' katika shughuli hiyo, hapo unatandikia ngozi kwa mbele ya jiwe ili visagwavyo visimwagikie chini. Kweli ya kale ni dhahabu. Hongera 'Wahadzabe' kwa kuendelea kudumisha mila zetu za jadi tangu dahari hizo zilizopitikia.
ReplyDelete