Na Benedict Liwenga, Maelezo.

Kiongozi wa Chama cha Kisoshalisti kilichojulikana kama “NAZI” Adolf Hitler (1889-1945) alikuwa mmoja kati ya Madikteta dhalimu na mwenye nguvu kuwahi kutokea katika karne ya 20. 

Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia mbabe huyo aliamka kwa nguvu kupitia Chama hiko cha Wafanyakazi wa Ujerumani na kuchukua udhibiti wa Serikali ya Ujerumani mnamo mwaka 1933.

Hitler aliamuru uanzishwaji wa kambi za mateso dhidi ya Wayahudi na makundi ya watu wengine huku akiamini kuwa kufanya hivyo ilikuwa chachu na tishio tosha dhidi ya ukuu wa himaya ya Aryani na hatimaye kusababisha vifo vya zaidi ya Wayahudi wapatao milioni Sita.

Mashambulizi ya Ujerumani dhidi ya nchi ya Poland mwaka 1939 ndiyo yaliyoanzisha Vita Kuu ya Pili ya Dunia ambapo mpaka kufikia mwaka 1941Ujerumani iliteka sehemu kubwa ya ardhi ya Ulaya na Afrika Kaskazini. 

Ili kuepuka kukamatwa kwa kukwepa utumishi katika jeshi la Austria-Hungary, Adolf Hitler aliondoka toka Vienna na kuelekea Munich mnamo Mei 1913 lakinibaadaye alilazimika kurudi tena.

Taarifa za kihistoria zinasema kuwa Kiongozi huyo wa Nazi alijiunga na jeshi la Bavaria na kuanza kufanya kazi za kujitolea ambapo mwaka uliofuata alishiriki kikamilifu katika vita ya Kwanza ya Dunia akiwa mstari wa mbele upande wa Magharibi ambapo uzoefu wake katika vita na mapambano uliathiri mawazo, fikra na mitazamo yake yote baada ya hapo.

Baada ya Vita Kuu ya kwanza ya Dunia, Hitler alichukua udhibiti wa chama hiko cha wafanyakazi wa Ujerumani kama kiongozi hivyo alitumaini kingemwezesha kushika dola ya Ujerumani punde si punde.

Aliposhindwa kwenye jaribio la Mapinduzi la mwaka 1923 yeye na wenzake walikamatwa na kufungwa jela na baada ya kutoka jela alijitahidi kukijenga chama hiko na kuanza mikakati ya kukamata dola kwa njia zilizo halali.

Hitler alikusudia kufanya mageuzi na kuendesha sera za kibaguzi ambazo zingetoa nafasi ya kutosha kwa Wajerumani kuweza kuishi katika himaya kubwa duniani.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 02, 2016

    Pamoja na ubaya wake mimi namzimia sera zake za kufufua uchumi,mpaka leo Ujerumani inazalisha bidhaa imara
    tungefuata sera zake za uchumi tutafika mbali.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...