Mkuu wa Kitengo wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. wengine ni wanachama wa Simba sport Club.
 Balozi wa Amani wa Simba, Risasi Mwaulanga akizungumza kuhusiana na wanachama na mashabiki wa Simba kwenda kuishangilia timu ya Yanga katika mchezo utakaochezwa katika uwanja vya Taifa jijini Dar es Salaam. kulia ni Mkuu wa Kitengo wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BALOZI wa Amani wa Simba, Risasi Mwaulanga amewataka Wanachama wa Simba na wapenzi wa mpira wajitokeze kwa wingi siku ya kesho kwa ajili ya kuishangilia na kuisapoti Timu ya Yanga katika mchezo wao wa kombe la Shirikisho Afrika CAF dhidi ya TP Mazembe utakaopigwa kwenye dimba la Uwanja wa Taifa. Wanachama hao wa Simba kutoka Wilaya ya Temeke wamesema kuwa uzalendo unatakiwa kuwekwa mbele na wao kama wapenda soka basi hakuna budi kuweza kuishangilia Yanga kwani kama wakifanya vizuri nchi itajitangaza.

Amesema kuwa, kuna wanachama wengi wa Simba ambao watajitokeza kwa wingi kuweza kuisapoti Yanga katika mchezo huo pia wanaamini kuwa kama watafanya vizuri na kuchukua kombe hili basi wataongeza timu katika michuano ya kimataifa. "Tunapocheza kwenye mechi za ligi tunakuwa na ushindani ila wakati mtani wetu anacheza mechi za kimataifa ni lazima tuonyeshe uzalendo na kuishangilia kwa juhudi zetu zote ili iweze kufanya vizuri,".

Naye Mkuu wa Kitengo wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro amesema kuwa anafurahishwa sana na hatua ya wanachama hao kuja kuisapoti timu yao hasa katika kipindi hiki cha michuano ya kimataifa na zaidi mafanikio ya Yanga yataitangaza zaidi nchi.  "Tunawashukuru wanachama wa Simba kwa kujitikeza kuja kuunga mkono timu yetu kwenye michuano ya kimataifa na sisi tunaungana nao pia tunapenda kuwaomba radhi Wanachama wa Simba na uongozi kwa ujumla kwa kitendo cha wanachama wetu miaka ya nyuma kwa kuwashangilia TP Mazembe na kitendo hicho hakitajirudia tena,"amesema Muro.

Amewaomba wanachama wa Yanga kujitokeza kwa wingi na wakivaa jezi zao pamoja na timu zingine kuja kuisapoti Yanga na amemshukuru aliyekuwa Rais Wa Simba Ismail Aden Rage kwa hatua aliyoionesha kwa kuisapoti katika kipindi chote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...