Mkurugenzi wa Mobisol Tanzania Henrik Axelsson (Kushoto) akionyesha vifaa mbalimbali vinavyozalishwa na kampuni hiyo wakati wa ufunguzi wa huduma zake wilayani Bagamoyo hivi karibuni. 

Imefanikiwa kufikisha huduma wa wateja robo milioni kanda Afrika Mashariki Kampuni kutoka nchini Ujerumani inayotoa huduma ya kusambaza umeme wa jua na kuuza vifaa vyake imeweza kubadilisha maisha ya familia robo milioni maeneo ya vijijini kuwa na maisha ya kisasa kutokana na kufikiwa nishati ya umeme katika nchi za Rwanda,Tanzania na Kenya. 

 Mobisol,kampuni ya Kijerumani inaoongoza kwa kutoa huduma za umeme wa jua imeweza kufunga umeme wa nishati ya jua kwa familia 50,000 ikiwemo sehemu za biashara katika maeneo wanayoishi wananchi wenye vipato vya chini ambao hawajafikiwa umeme wa gridi ya taifa kwenye nchi za Tanzania,Rwanda na Kenya. Kupitia mpango wake maalumu wa kukopesha unaowawezesha wateja kufanya malipo kwa awamu kupitia simu za mkononi yanaochukua kipindi mpaka kufikia hadi miaka mitatu, wananchi wengi wenye vipato vya chini wameweza kujiunga na kuufurahia mpango huu.Mteja anatakiwa kulipia shilingi 999 kwa siku ambapo akikamilisha malipo atapata umeme wa uhakika wenye nguvu zinazoanzia 80W hadi kufikia 200W kulingana na mahitaji yake kwa matumizi ya vifaa vya nyumbani. 

 Meneja Masoko wa Mobisol Tanzania,Allan Rwechungura amesema jijini Dar es Salaam kuwa mbali na wateja kuunganishiwa umeme wa jua kwa mpango unaoleta unafuu mkubwa pia wanaweza kujipatia vifaa bora vya matumizi kama vile mashine za kukata nywele,vifaa vya muziki (Music system),pasi,feni na vifaa vinavyoweza kuwaongezea wateja vipato mfano chaji maalumu ya kuchajisha simu kibiashara.

 “Mobisol ni mkombozi wa kuondoa tatizo la umeme kwa wateja wasio na uwezo wa kununua vifaa vya kufungiwa umeme wa jua kwa mara moja kwa gharama zinazofikia Dola za Kimarekani 800 ila imewawekea mpango maalumu unaowawezesha kulipia huduma hii kwa awamu.

Dhamira yetu ni kuona huduma hii inaleta mabadiliko kwenye jamii kwa kuboresha maisha ya wananchi na sio kuwasha taa tu ama kuchaji simu”Alisema. Aliongeza kuwa kampuni inatoa ofa ya kufuatilia iwapo wateja wake wanapata huduma ya uhakika kwa kipindi cha miaka mitatu na iwapo kunakuwepo na matatizo yanarekebishwa na wataalamu wake waliobobea katika ufundi wa mitambo inayozalisha umeme wa jua,dhamira kubwa ikiwa ni kubadilisha maisha ya wakazi wa maeneo ambayo hayajafikiwa umeme wa gridi ya taifa hususani maeneo ya vijijini kuwa bora. 

 Rwechungura alisema moja ya malengo ya kampuni pia ni kuwawezesha watoto wanaosoma shule maeneo ya vijini kuweza kujisomea kwa kutumia mwanga wa umeme,kuweza kusikiza redio , kuangalia televisheni na kuperuzi kwenye internet ili wapate taarifa na fursa ya kuelimika “Uwekezaji wetu kwenye sekta hii vilevile umejikita katika utunzaji wa mazingira ikiwemo kuboresha maisha ya wananchi kwa kuwawezesha kufanya shughuli mbalimbali za kuwaongezea vipato kupitia uzalishaji unaofanyika kwa kutumia nishati ya umeme”. 

 Wakati huohuo Rwechungura ameeleza kuwa kwa mara ya kwanza kampuni ya Mobisol itashiriki katika Maonyesho ya kimataifa ya Biashara maarufu kama SabaSaba yanayotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu.Maonyesho hayo ya biashara yatawawezesha wananchi kujua huduma zinazotolewa na kampuni ya Mobisol nchini ikiwemo kununua bidhaa za kampuni hususani Televisheni bora zenye ukubwa tofauti ambazo zimekuwa zikiwavutia wateja wengi. “Televisheni ni kifaa pekee kinachowawezesha kupatikana taarifa , burudani na kinachounganisha jamii,wakazi wa vijijini kupitia televisheni wanaweza kuunganishwa na dunia nzima,wanahitaji kuishi maisha ya kisasa na sisi tupo kwa ajili ya kubadilisha maisha ao kuwa bora”.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...