Na Zainab Nyamka, 
Globu ya Jamii.
KIKOSI cha Yanga kipo tayari kuwavaa TP Mazembe leo  katika mchezo wa pili wa kombe la Shirikisho Afrika ambapo unatarajiwa kupigwa katika dimba la uwanja wa Taifa huku wachezaji wote wakiwa katika hali nzuri kimchezo na kisaikolojia. 
Hayo yamesemwa jana  katika mkutano na waandishi wa habari kuwa Wachezaji wapo tayari kwa ajili ua ushindi.
Mkuu wa Kitengo cha habari na Mawasiliano Jerry Muro amesema kuwa, kwa sasa kilichobakia ni kusubiri muda ufike na kwa maelezo ya kocha mkuu Hans Van De Pluijm amehakikishia wanachama wa Yanga kuwa watapambana hadi hatua ya mwisho.
" Kocha mkuu amesema kuwa wachezaji wote wapo sawa na watapambana hadi hatua ya mwisho na wamewahakikishia benchi la ufundi kuwa wapo uwanja wa nyumbani na watautumia vizuri,".
Muro amesema kuwa, msimamizi wa mechi hiyo amewataka viongozi wa Yanga kuhusiana na mechi ya leo katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwa  una uwezo wa kuchukua watu 60,000, lakini  utafungwa wakati wa mchezo wa Yanga na TP Mazembe ya DRC baada ya mashabiki 40,000 kuingia.

Hayo ni maagizo ya Kamisaa wa mchezo huo wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika, ambao mashabiki wataingia bure, Celestine Ntangungira kutoka Rwanda.
Sasa Mabingwa hao wa Tanzania Bara watashuka ili  kupigana kuonyesha hawapotezi mchezo wa nyumbani,  hasa baada ya ule wa awali kupoteza nchini Algeria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...