Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Baada ya ushindi wa  goli 2-0 dhidi ya Mwadui FC, timu ya Azam imeingia kambini kujiandaa na mchezo wa kombe la Shirikisho (ASFC) utakaopigwa siku ya Ijumaa katika uwanja wa Azam Complex.

Azam wanatarajiwa kukutana na Mtibwa kwenye mchezo wa ASFC ijumaa ambapo awali mchezo huo ulipangwa kucheza saa moja usiku, na badala yake utapigwa saa kumi alasiri.

Msemaji wa Azam, Jafari Iddy ametabanaisha kuwa baada ya mchezo wa jana dhidi ya Mwadui wameingia rasmi kambini kwa ajili ya kujiandaa na mechi dhidi ya Mtibwa ambao ni moja mechi ngumu kwani inahitaji matokeo chanya kwa kila upande ili kuweza kuendelea katika hatua ya nane bora kwenye michuano hiyo.

Chini ya kocha Mromania Aristica Cioaba imejizatiti kutoka na ushindi kwenye mchezo huo kwani itakua ni njia mojawapo ya kuweza kushiriki michuano ya kimataifa na hilo ndiyop lengo kuu la klabu hiyo.

Mbali na mechi hiyo, Azam pia wanakabiliwa na mechi ya kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Mbabane Swallows utakaopigwa kwenye uwanja wa Azam Complex Machi 12.


Msemaji wa Azam, Jafari Iddy

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...