Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Ashatu Kijaji jana amekutana na wafanyabiashara Jijini Mwanza kwa ajili ya kusikiliza na kutatua baadhi ya kero za kibiashara kutoka kwa wafanyabiashara hao chini ya chama chao cha TCCIA.
Dkt.Kijaji aliwahakikishia wafanyabiashara hao kwamba serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kufanyia biashara huku akibainisha kwamba mashine za kutolea stakabadhi EFD's sasa zinatolewa na Mamlaka ya Mapato nchini TRA na hivyo wafanyabiashara hao wataondokana na baadhi ya kero walizokuwa wakikumbana nazo kutoka kwa mawakala wa mashine hizo ikiwemo kuzinunua kwa bei kubwa.
Awali wafanyabiashara hao walilalamikia suala la machinga kupanga bidhaa zao kando ya milango ya maduka yao ambapo Naibu Waziri Kijaji aliwasihi kuwa na subira wakati serikali utaratibu wa kuwasajili na kuwapatia machinga vitambulisho kama ilivyoelezwa kwenye bajeti ya mwaka 2017/18 na hatimaye kuwaboreshea maeneo yao ya kufanyia biashara. Na Binagi Media Group


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Ashatu Kijaji (aliyesimama), akizungumza na wafanyabiashara Jijini Mwanza jana. Wengine ni Meneja wa TRA Mkoa wa Mwanza, Ernest Dundee (wa kwanza kushoto), Injinia Boniphace Nyambele aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (wa pili kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo TCCIA mkoa wa Mwanza Elibariki Mmari (kulia).

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo TCCIA mkoa wa Mwanza Elibariki Mmari, akizungumza kwenye kikao hicho
Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria kikao hicho akiwemo Makamu wa Rais wa TCCIA, Joseph Kahungwa (kushoto)

Baadhi ya wafanyabiashara Jijini Mwanza ambao walihudhuria kikao cha majadiliano baina ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Ashatu Kijaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...