THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

KICK OFF YOUR DAY WITH MICHUZI BLOG, MOST READ SWAHILI BLOG ON EARTH!


EID MUBARAK MDAU WA GLOBU YA JAMII POPOTE PALE ULIPO

video


Swala ya Eid el Fitr iliyofanyika Bustani ya Mnazi Mmoja Dar es salaam leo


Eid El Fitr uwanja wa samora mjini iringa leo

Waumini  wa  dini ya kiislamu mjini  Iringa  wakiwa katika ibada ya Eid el Firt  uwanja wa Samora  leo
Ibada ya   Eid ikiendelea katika uwanja wa Samora mjini Iringa  leo 
Wazee maarufu na makada  wa  CCM ambao ni waumini wa dini ya Kiislam  wakipiga picha ya pamoja na mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Abed Kiponza  kulia  wa pili  kulia ni Mr  Mbata
Khutba baada ya SWala ya Eid el Fitr uwanja wa Samora mjini Iringa leo.
Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA


Swala ya Eid el Fitri iliyoswaliwa kitaifa katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Zanzibar leo asubuhi

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa nne kulia) akijumuika na Waislamu mbali mbali na Viongozi katika Swala ya Eid el Fitri iliyoswaliwa kitaifa katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Zanzibar  leo asubuhi katika kusherehekeka mfunguo wa Mwezi Mtukufu wa  Ramadhan
 Baadhi ya Mashekhe na Vingozi wakijumuika na waumini mbalimbali na Viongozi katika Swala ya Eid el Fitri iliyoswaliwa kitaifa katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Zanzibar  leo asubuhi katika kusherehekeka mfunguo wa Mwezi Mtukufu wa  Ramadhan
 Baadhi ya waislamu waliomaliza Swala ya Eid el Fitri wakimasikiliza Sheikh Mziwanda  Ng'wali  Ahmed  (hayupo pichani ) alipokuwa akitoa Khutba baada ya swala hiyo ambapo aliwataka waislamu kusherehekea Sikukuu ya Eid kwa upendo na mashirikiano katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Zanzibar  leo asubuhi 
 Sheikh Mziwanda  Ng'wali  Ahmed (aliyesimama) akitoa Khutba baada ya Swala ya  Eid el Fitri mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein na Viongozi mbali mbali wa Kitaifa na Wailslamu waliojumuika kwa pamoja katika viwanja  vya Maisara Suleiman Mjini Zanzibar leo asubihi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Watoto walioshiriki katika Swala ya Eid el Fitri na kuwatakia Kheri katika kusherehekea Sikukuu hii ya  kumaliza mfungo wa Mwezi Mtukufu wa  Ramadhan.
Kwa picha zaidi za Baraza la Eid BOFYA HAPA


JK katika Swala ya Iddi Dar es Salaaam

 Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wakiswali sala ya Iddi El Fitr katika masjid Maamur Upanga jijini Dar es Salaam leo asubuhi
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu muda mfupi baada ya kuswali sala ya Iddi El Fitr katika mshikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
 "...Eid Mubarak....Eid Mubarak..."
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mlemavu mara baada ya kumalizika kwa swala ya Iddi katika masjid Maamur Upanga jijini Dar es Salaam leo asubuhi.


Swala ya Eid El Fitr kitaifa yaswaliwa kwenye viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar leo

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal (katikati),Sheikh Mkuu,Issa Shaaban Simba,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Sheikh Mussa Salum wakijumuika na Waumini wengine wa Dini ya Kiislam kwenye Swala ya Eid El Fitr iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja,Jijini Dar es Salaam leo.Picha zote na Othman Michuzi.Sehemu ya Waumini wa Dini ya Kiislam wakiwa kwenye Ibada ya Eid el Fitr katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
 Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam,Sheikh Mussa Salum akitoa Khotuba katika Idada ya Swala ya Eid El Fitr iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja,Jijini Dar es Salaam leo.
 Mawaidha yakiendelea mara baada ya Swala ya Eid el Fitr.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akitoa salamu za Eid el Fitr leo mara baada ya Swala iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja,Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Ulinzi,Dkt. Hussein Mwinyi (katikati) akijumuika pamoja na Waumini wenzake wa Kiislam katika Swala ya Eid El Fitr iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja,Jijini Dar es Salaam leo.


WAFANYAKAZI WAISLAMU WA VODACOM TANZANIA NA MARAFIKI ZAO WATOA MSAADA KITUO CHA YATIMA

 Watoto wanaolelewa katika kituo cha yatima cha Umra kilichopo Magomeni jijini Dar es Salaam, wakiangalia simu ya mfanyakazi wa  Vodacom Tanzania Shamsa Hamud(anaewashuhudia)Wafanyakazi wa kampuni hiyo walifika kituoni hapo kwa ajili ya kutoa msaada wa vyakula mbalimbali na fedha taslimu zilizochangwa na wafanyakazi waislamu na marafiki zao kwa ajili ya watoto hao kusherehekea sikukuu ya Idd.
 Watoto wanaolelewa katika kituo cha Yatima cha Umra kilichopo Magomeni jijini Dar es Salaam, wakifurahia moja ya zawadi walizopewa msaada na Wafanyakazi wa Kiislamu na marafiki zao  wa Vodacom Tanzania, Vikiwemo vyakula mbalimbali na fedha tasilimu kiasi cha shilingi 380,000 kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Idd 
  Iman Abdalah (wapili kushoto) wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Umra akiongoza swala  kwa ajili ya watoto wenzake kuwashukuru wafanyakazi wa Kiislamu na marafiki zao wa Vodacom Tanzania waliowachangia vitu mbalimbali vikiwemo vyakula na fedha taslimu Tsh 380,000. Kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Idd.Kushoto ni mfanyakazi wa kampuni hiyo  Shomari Shomari na kulia ni Salum Mwalim.

 Mfanyakazi wa Vodacom  Tanzania ,Shomari Shomari akimkabidhi fedha taslimu kiasi cha Tsh 380,000 Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto Yatima cha Umra kilichopo Magomeni jijini Dar es Salaam,Bi.Rahma Kishumba,Fedha hizo zilichangwa na wafanyakazi waislamu wa kampuni hiyo na marafiki zao kwa ajili ya kuwanunulia viatu vya sikukuu ya Idd watoto wa kituo hicho.
 Mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha yatima cha Umra Iman Abdalah ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza  akipokea msaada wa ndoo ya mafuta ya kupikia kutoka kwa Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Yessaya Mwakifulele wakati walipopelekewa msaada wa vitu mbalimbali na fedha taslimu kiasi cha Tsh 380,000 zilizochangwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo na marafiki zao kwa ajili ya watoto hao kusherehekea sikukuu ya Idd,Kulia ni Salum Mwalim.
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,Shomari Shomari (kushoto) na Salum Mwalim(kulia) wakiwakabidhi moja ya gunia la mchele watoto wanaolelewa katika kituo cha Yatima cha Umri kilichopo Magomeni Jijini Dar es Salaam kwa ajilia ya kusherehekea sikukuu ya Idd, Jumla ya Vitu mbalimbalikii ikiwemo fedha taslimu kiasi cha Tsh 380,000.zilizochangwa na wafanyakazi wa Kiislamu wa Vodacom na marafiki zoa vilitolewa msaada katika kituo hicho.


DKT BILALI AONGOZA SWALA YA IDDI KITAIFA MNAZI MMOJA DAR ES SALAAM LEO

 Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal (nyuma ya Shehe anayeswalisha) akijumuika na waumini wa Kiislamu kwa Swala ya Iddi Kitaifa iliyofanyika katika Bustani ya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam asubuhi ya leo.
Sehemu ya waumini wa Kiislamu katika Swala ya Iddi Kitaifa iliyofanyika katika Bustani ya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam asubuhi ya leo.


salamu za eid kutoka kwa Dekula kahanga vumbi wa sweden


President Obama participates in a town hall at the Summit of the Washington Fellowship for Young African Leaders

The President participates in a town hall at the Summit of the Washington Fellowship for Young African Leaders. The three-day Summit will cap off the Washington Fellowship, the flagship program of the President’s Young African Leaders Initiative (YALI), and give 500 of sub-Saharan Africa’s most prominent young leaders the opportunity to engage with U.S. government officials, entrepreneurs and civil society representatives as well as leaders in international development. Courtesy of The White House
 Arumeru East Member of Parliament Hon. Joshua Nassari with fellow participants rejoice the moment 
 President Obama fields questions from  participants
President Obama responds to a question. Below the US President shakes hands and bids farewell to the participants. For more photos CLICK HERE


zawadi ya eid toka kwa hafsa kazinja


KAGASHEKI CUP 2014 - KAGONDO FC WATINGA NUSU FAINALI KWA KUIFUNGA IJUGANYONDO KWA MIKWAJU YA PENATI 4-3

Wachezaji wa Timu ya Kagondo Fc wakimpongeza mchezaji wao aliyewapa ushindi wa kwenda hatua ya Nusu fainali Abdallatifu Khamis juu kwa juu.
Kufungwa kubaya!!! Wachezaji wa Timu ya Ijuganyondo wakitoka Uwanjani wakiwa hawana hamu. Kwa picha zaidi na Faustine Ruta BOFYA HAPA


EID MUBARAK kutoka CCM california

 

Chama Cha Mapinduzi Tawi la California, Kinawatakia Kheri na Baraka Waislamu wenzetu wa hapa na dunia kote katika sherehe hii muhimu ya EID MUBARAK.
 
Tunaomba kupitia sherehe hizi amani na upendo vitawale na Mungu azidi kutujalia  huruma,nguvu na maisha marefu.
 
Tuko pamoja katika shamrashamra.
 
HAPPY EID EL-FITR
KHERI YA IDD EL-FITR


FAMILIA YA MAREHEMU MWESIGWA BLANDESI YATOA SHUKRANI


Wapendwa Jamaa, marafiki na Watanzania wenzetu kwa ujumla,


Familia ya Marehemu Mwesigwa Blandesi kwa pamoja na familia ya Byorwango hapa California,
Tunapenda kutoa shukrani za dhati  naza kipekee kwa wote mlioshiriki kikamilifu katika njia zote za mwanzoni mpaka mwishoni mwa maisha ya marehemu Blandesi Mwesigwa aliyefariki May 26 2014.

Tunashukuru mengi, kuanzia, mchango ya matibabu, ushirikiano wa kuuguza, sala, mawazo, na kuwa pamoja na kwa ukaribu katika shughuli zote za msiba mojawapo kubwa ikiwa ni kusaidia kwa hali na mali shghuli yote ya msiba kuanzia hapa Marekani mpaka Tanzania-Bukoba ikafanikiwa vizuri na kuweza kumpumzisha vyema rafiki yetu, ndugu yetu na kiongozi wetu mpendwa.
Tumetiwa moyo sana na kufarijika sana kwa haya yote na hili limekuwa jambo la muhimu sana kwetu sisi pamoja na wengine wote kujifunza umuhimu wa kuwa karibu na watu kuwa katika jumuiya kwa ujumla. Kupitia hii shida iliyotupata wote tumejifunza na kujihakikishia kuwa Marehemu alikuwa kioo na nguzo kwa jamii na familia kwa maisha aliyoyaishi.
Tunashukuru sana uongozi mzima wa TCO chini ya bodi, tunashukuru vikundi vya makanisa ilikiwemo Ressurection Lutheran Church la Oakland, pia tunashukuru vyama vya siasa kikiwemo CCM, na pia jumuiya mbali mbali za nchi mbalimbali hapa America. Juu ya yote tunashukuru Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani chini ya uongozi mahili wa Balozi wetu Mheshimiwa L. Mulamula kwa jitihada zao za kila aina katika kusaidia na kutuongoza kwa mambo mbalimbali.
Tunashukuru watu waliopangiwa shughuli kwenye makundi mbalimbali: Kupika, power-point, ukusanyaji wa pesa, masuala ya imani, ratiba, utumbuizaji, na mengine mengi ambayo ni mengi na ni vigumu kuyataja yote.
Mwili wa ndugu yetu Marehemu Mwesigwa ulisindikizwa na wanafamilia akiwemo mke wake Rosemary Blandesi na watoto na baadhi ya wanafamilia.
Tulifika salama Bukoba Tanzania na kufanya mazishi siku ya Jummane (June 10th 2014) yaliyojumuisha watu wengi sana wakiwemo wenzetu tuliowahi kukaa nao hapa  California na kwa sasa wako Tanzania: Mbakileki Mutahaba, Lyidia Mutahaba, Dawson Ndyetabula, waliosafiri kutoka Dar es Salam, Mama Julie Mkenda (Mama Pricilla) kutokea Arusha na  ujumbe mwingine kutoka Kenya ulioongozwa na rafiki mkubwa wa Marehemu Ndugu Kibunguchi pamoja na ndugu wengine wengi walioacha shughuli zao na kufika nyumbani kwa marehemu kwa ajili ya kutoa pole kule Bukoba.  Mliwakilishwa vizuri na tunawashukuru.
Tunaleta salamu nyingi sana za Shukrani kwenu wote kutoka kwa familia zetu hizi mbili huko Tanzania kwa yote mliyoyafanya mpaka marehemu anafikishwa kwenye makazi ya milele. Hawana cha kuwapa cha kuonyesha shukrani zaidi, ila tu kuwaombea kwa mwenyezi Mungu awaongezee upendo, ushirikiano na amani katika Umoja wetu na Jamii yetu kwa ujumla.
Tumerudi salama na tayari tunaendelea na majukumu yetu ya kawaida.  Wale ambao wangependa kututembelea basi wote mnakaribishwa na tunaweza kubadilishana habari mbali mbali za mambo yalivyokwenda pale nyumbani kwa Rosemary Blandesi -Tracy.
Tunazidi kuwashukuru sana na kuwaombea kwa Mungu awajali mema yote ikiwemo baraka na afya.
Mwenyezi Mungu azidi kuilaza roho 
ya Marehemu mahali pema peponi
 AMINA.

Erick Byorwango 
Mwakilishi wa familia.


swala ya Iddi mkoani arusha leo

 Sheikh wa mkoa wa Arusha Shaban bin Jumaa akitoa hutuba ya Idd kwa waumini wa dini ya kiislamu na kuwataka kudumisha amani na mshikamano miongoni mwa waumini wa dini nyingine ilikuweka katika hali ya utlivu mkoa wa Arusha ilikuweza kujiletea maendeleo endelevu kama mafungisho ya dini yanavyowataka
Waumini wa dini ya kiislamu wakihitimisha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani wakiwa kwenye ibada ya swala ya Iddy el Fitry kwenye uwanja wa sheikh Amri Kaluta Abeid jijini Arusha. Picha na  Mahmoud Ahmad wa Globu  ya Jamii, Arusha


Was Your Ramadan Accepted? ~ Sheikh Said Rageah


mambo ya gado

Fraudulent Tycoon Somaia Jailed in UKBENKI YA EXIM YAWAANDALIA FUTARI WATEJA WAKE ZANZIBAR


Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko wa Zanzibar, Mhe. Nassor Mazrui (kulia) akizungumza wakati wa Iftari iliyoandaliwa na Benki ya Exim Tanzania Tawi la Zanzibar kwa ajili ya wateja wake hivi karibuni. Wengine kulia kwake ni baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo na wateja walioalikwa katika tukio hilo. 
 Baadhi ya wafanyakazi na wateja wa Benki ya Exim Tanzania wakijumuika pamoja akatika Iftari iliyoandaliwa na benki hiyo Visiwani Zanzibar kwa ajili ya wateja wake


BREAKING NYUUUZZZZZ: VIONGOZI WA CHUO NA HOSPITALI YA IMTU WATINGA MAHAKAMANI, DPP AWAONDOLEA MASHTAKA

Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP), aliwapandisha kizimbani vigogo wanne wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba (IMTU) na baadaye kuwaondolea mashitaka kupitia hati ya Nole ya kuwaondolea mashtaka ya kushindwa kufukia viungo vya binadamu na kupeleka hati ya kufukia viungo vilivyotumika kufundishia kwa Kampuni Coroner. 
 Vigogo hao ni, Venkat Subbaian (57), Appm Shankar (64), Prabhakar Rao (59) na Dinesh Kumar (27) ambao walisomewa mashtaka yao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo  saa 8:07  mchana.  Washtakiwa hao walisimama kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kwey Lusemwa. 
Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Magoma Magina alidai kuwa Julai 20, mwaka huu washtakiwa wakiwa na nyadhifa  tofauti, Profesa, Mtawala na wahadhiri, kwa makusudi walishindwa kufukia mifuko 83 iliyokuwa na viungo vya binadamu kinyume cha sheria ya 128 kifungu cha 8 na cha 9 cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA). 
 Magina alidai kuwa katika shitaka la pili, washtakiwa wote kwa pamoja walishindwa kupeleka hati ya kumtarifu kwamba wamefukia viungo hivyo baada ya kutumika kufundishia kama sheria inavyowataka. Hakimu Lusemwa alisema washtakiwa watakuwa nje kwa dhamana kwa kuwa na wadhamini wawili raia wa Tanzania kila mmoja. 
Hata hivyo, kabla mahakama haijasikiliza kipengele cha dhamana, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Salum Ahmed aliwasilisha hati ya Nole kutoka kwa DPP akidai kuwa anawaondolea vigogo hao mashtaka na kwamba hana nia ya kuendelea kuwashitaki. 
 Ahmed alidai kuwa DPP anawaondolea washtakiwa mashitaka hayo chini ya kifungu cha 91 kidogo cha (1) cha CPA kwa kuwa hana nia ya kuendelea kuwashitaka. 
 Wakili wa washtakiwa Gaudiosus Ishengoma alisema kwamba inaonekana kuna mbinu kubwa dhidi ya washtakiwa. Alisema anavyofahamu kwamba hati ya mashitaka ingekuwa na kasoro wateja wake wangepata dhamana na baadaye ingewezekana kubadilishwa. 
Alisema kutokana na sababu hiyo, ana wasiwasi kwamba inawezekana DPP ana nia ya kuwafungulia wateja wangu kesi yenye mashitaka yasiyokuwa na dhamana ili wakasote mahabusu. 
 Viwanja vya mahakama hiyo vilikuwa tulivu huku wanaodaiwa kuwa wafanyakazi wa IMTU wakiwa wamesimama katika makundi makundi wakijadiliana hili na lile. 
Kupitia magari ya Jeshi la Polisi, T 366 AVG aina ya Rav4 alipanda mshtakiwa wa tatu kwa madai kuwa ni mgonjwa na washtakiwa wengine waliondoka mahakamani hapo katika gari yenye namba za usajili KX06EFY aina ya Toyota Landcruiser na kurudishwa mahabusu ya jeshi hilo.
 Washtakiwa wakiwa katika gari la polisi 
 Wakipanda gari baada ya kusomewa mashitaka
 Wakitoka mahakamani baada ya kusomewa mashitaka
 
Washtakiwa wakisubiri kuingia mahakamani.
Picha na Sultani Kipingo wa Globu ya Jamii


SALAMU ZA EID KUTOKA KWA PAPAAA HASSANI KANIKI MUTU YA KILO YA TRANSHPOO

Nikiikala hapa ku Daresalama ninawaombea wato nyote sikukulu nyema yenye furaha na upendo. Hivi sasa nalikuaga kutayarishaga singo yangu mupya kwa ajiri ya Iddi hii, lakini produza akasemaga ana makazi bwerere ya kina Dayamond na Omi Dimpoz hivyo singo yangu itaitokaga kunako mwezi wa kenda. Haina neno lakini Iddi jema ku wato nyote.


SALAAM ZA EID KUTOKA MASSACHUSETTS, MAREKANI

Familia ya Kibodya inawatakia Waislam wote Dunia Eid Mubarak njema yenye amani na upendo tuendeleze yote mema tullyofanya kwenye mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan


salamu za iddi kutoka kwa wanalibeneke wa Bukoba wadau

#‎BUKOBAWADAU‬ BLOG inakutakia sikukuu njema ya Eid-el-Fitr popote pale ulipo, na inawapongeza waumini wote wa dini ya Kiislamu kwa kukamilisha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.


MKUTANO WA MAJADILIANO KUHUSU UFADHILI WA MIRADI YA MAENDELEO KATI YA SERIKALI YA TANZANIA NA JAPAN KWA MWAKA 2014/2015.

Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip I. Mpango (wa pili kushoto) akifungua mkutano wa majadiliano baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Japan kuhusu ufadhili wa miradi ya maendeleo kwa mwaka 2014/15.katika ukumbi  wa mikutano wa Wizara ya Fedha na yaliratibiwa na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
Wajumbe kutoka Serikali ya Tanzania wakifuatilia michango mbalimbali kutoka kwa wajumbe wa mkutano huo. Miradi iliyowasilishwa ilihusisha Sekta za Kilimo, Viwanda, Usafirishaji, Nishati, Maji, na Afya.
 Wajumbe wa mkutano uliohusisha Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wa Wizara, Wakurugenzi na Wataalam wa Sekta mbalimbali wakifuatilia kwa makini majadiliano yaliyokua yakiendelea.
 Wajumbe kutoka Serikali ya Tanzania wakifuatilia michango mbalimbali kutoka kwa wajumbe wa mkutano huo. Miradi iliyowasilishwa ilihusisha Sekta za Kilimo, Viwanda, Usafirishaji, Nishati, Maji, na Afya.
 Wajumbe kutoka Serikali ya Japan wakichukua mambo ya muhimu wakati Mkutano wa Majadiliano ulipokuwa ukiendelea. Ujumbe huo uliongozwa na Balozi wa Japan nchini Tanzania Bw. Masaki Okada.
Picha na: Thomas Nyindo, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.