Wapendwa Jamaa, marafiki na Watanzania wenzetu kwa ujumla,


Familia ya Marehemu Mwesigwa Blandesi kwa pamoja na familia ya Byorwango hapa California,
Tunapenda kutoa shukrani za dhati  naza kipekee kwa wote mlioshiriki kikamilifu katika njia zote za mwanzoni mpaka mwishoni mwa maisha ya marehemu Blandesi Mwesigwa aliyefariki May 26 2014.

Tunashukuru mengi, kuanzia, mchango ya matibabu, ushirikiano wa kuuguza, sala, mawazo, na kuwa pamoja na kwa ukaribu katika shughuli zote za msiba mojawapo kubwa ikiwa ni kusaidia kwa hali na mali shghuli yote ya msiba kuanzia hapa Marekani mpaka Tanzania-Bukoba ikafanikiwa vizuri na kuweza kumpumzisha vyema rafiki yetu, ndugu yetu na kiongozi wetu mpendwa.
Tumetiwa moyo sana na kufarijika sana kwa haya yote na hili limekuwa jambo la muhimu sana kwetu sisi pamoja na wengine wote kujifunza umuhimu wa kuwa karibu na watu kuwa katika jumuiya kwa ujumla. Kupitia hii shida iliyotupata wote tumejifunza na kujihakikishia kuwa Marehemu alikuwa kioo na nguzo kwa jamii na familia kwa maisha aliyoyaishi.
Tunashukuru sana uongozi mzima wa TCO chini ya bodi, tunashukuru vikundi vya makanisa ilikiwemo Ressurection Lutheran Church la Oakland, pia tunashukuru vyama vya siasa kikiwemo CCM, na pia jumuiya mbali mbali za nchi mbalimbali hapa America. Juu ya yote tunashukuru Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani chini ya uongozi mahili wa Balozi wetu Mheshimiwa L. Mulamula kwa jitihada zao za kila aina katika kusaidia na kutuongoza kwa mambo mbalimbali.
Tunashukuru watu waliopangiwa shughuli kwenye makundi mbalimbali: Kupika, power-point, ukusanyaji wa pesa, masuala ya imani, ratiba, utumbuizaji, na mengine mengi ambayo ni mengi na ni vigumu kuyataja yote.
Mwili wa ndugu yetu Marehemu Mwesigwa ulisindikizwa na wanafamilia akiwemo mke wake Rosemary Blandesi na watoto na baadhi ya wanafamilia.
Tulifika salama Bukoba Tanzania na kufanya mazishi siku ya Jummane (June 10th 2014) yaliyojumuisha watu wengi sana wakiwemo wenzetu tuliowahi kukaa nao hapa  California na kwa sasa wako Tanzania: Mbakileki Mutahaba, Lyidia Mutahaba, Dawson Ndyetabula, waliosafiri kutoka Dar es Salam, Mama Julie Mkenda (Mama Pricilla) kutokea Arusha na  ujumbe mwingine kutoka Kenya ulioongozwa na rafiki mkubwa wa Marehemu Ndugu Kibunguchi pamoja na ndugu wengine wengi walioacha shughuli zao na kufika nyumbani kwa marehemu kwa ajili ya kutoa pole kule Bukoba.  Mliwakilishwa vizuri na tunawashukuru.
Tunaleta salamu nyingi sana za Shukrani kwenu wote kutoka kwa familia zetu hizi mbili huko Tanzania kwa yote mliyoyafanya mpaka marehemu anafikishwa kwenye makazi ya milele. Hawana cha kuwapa cha kuonyesha shukrani zaidi, ila tu kuwaombea kwa mwenyezi Mungu awaongezee upendo, ushirikiano na amani katika Umoja wetu na Jamii yetu kwa ujumla.
Tumerudi salama na tayari tunaendelea na majukumu yetu ya kawaida.  Wale ambao wangependa kututembelea basi wote mnakaribishwa na tunaweza kubadilishana habari mbali mbali za mambo yalivyokwenda pale nyumbani kwa Rosemary Blandesi -Tracy.
Tunazidi kuwashukuru sana na kuwaombea kwa Mungu awajali mema yote ikiwemo baraka na afya.
Mwenyezi Mungu azidi kuilaza roho 
ya Marehemu mahali pema peponi
 AMINA.

Erick Byorwango 
Mwakilishi wa familia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...