Na Thomas William,Morogoro.
Usajili na Utambuzi wa watu katika mkoa wa Morogoro umezinduliwa rasmi Septemba 20, 2014 na Mkuu wa Mkoa wa huo, Joel Bendera katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Morogoro.
Usajili na Utambuzi wa watu katika mkoa wa Morogoro umezinduliwa rasmi Septemba 20, 2014 na Mkuu wa Mkoa wa huo, Joel Bendera katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Morogoro.
Akizindua zoezi hilo aliwasisitiza wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa mamlaka za
Serikali za Mitaa, makatibu tawala wilaya na viongozi wote kufikia ngazi ya kijiji
na mtaa kuhakikisha kwamba wanashiriki kikamilifu katika kufanikisha usajili wa
watu katika mkoa wake.
Alisema viongozi na watendaji wote katika mkoa huo wanatakiwa kuweka
uzalendo mbele katika suala hilo na kuhakikisha kwamba hakuna wageni
wanaopata vitambulisho vya taifa ambayo ni vya raia.
Zoezi hili ambalo linawahusu wananchi na wakazi wa wilaya zote za Morogoro
ambazo ni Morogoro Mjini, Morogoro Vijijini, Mvomero, Kilosa, Kilombero, Gairo,
na Ulanga wenye umri wa miaka 18 na zaidi linafanyika kwa siku saba.
Ili kusajiliwa mwombaji anatakiwa kufika katika kituo cha usajili ukiwa na nyaraka
muhimu zinakazokutambulisha mathalan, cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha
Mzanzibari Mkaazi, Cheti cha Elimu ya Msingi, Sekondari au Chuo, Leseni
ya Udereva, Kadi ya kupigia Kura, Pasipoti na Kadi ya Bima ya Afya. Wageni
wanatakiwa kuwa nakala ya Pasipoti ya nchi wanazotoka na kibali cha kuishi
nchini.
Aidha, mwombaji anakumbushwa kuhakikisha jina lake limesajiliwa katika rejesta
ya makazi iliyopo katika Serikali ya Mtaa/Kijiji kabla ya kuanza taratibu za usajili.
Vituo vitafunguliwa asubuhi saa 2:00 hadi saa 11:00 jioni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...