Timu ya Abajalo ya Sinza jijini Dar es Salaam imefanikiwa kukata tiketi ya fainali ya Dr Mwaka Sports Xtra NDONDO CUP 2014 baada ya kuifunga Burudani FC ya Temeke mikoroshini mabao 3-1. Mabao ya Abajalo kwenye mchezo huo yalifungwa na Idd Kulachi ‘Kleberson’ aliyefunga mabao mawili kati ya matatu. Mchezo huo wa nusu fainali ya pili ulipigwa kwenye uwanja Bandari uliopo maeneo ya Tandika Mwembe Yanga. Kwa ushindi huo sasa Abajalo itacheza na Tabata FC kwenye fainali itakayopigwa siku ya jumapili ya tarehe 30/11/2014 pale pale kwenye uwanja wa Bandari,huku timu za Black Six ya Buguruni na Burudani zikipambana kwenye mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu wa michuano hiyo iliyovutia mashabiki kibao mpaka sasa,Bingwa mwa mashindano hayo atapata pesa taslim shilingi milioni tano huku mshindi wa pili akipata milioni tatu na mshindi wa tatu akiambulia shilingi milioni mbili.Capture7

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...