WASANII 87 mahiri wa muziki wa Injili wa hapa nchini na nje ya nchi wamependekezwa na wadau washiriki kwenye miaka 15 ya Tamasha la Pasaka mwaka huu.
 
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Dar es Salaam leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa wadau wa muziki huo wameomba waandaaji wahakikishe wasanii hao wanakuwepo mwaka huu.
 
“Kama mnavyofahamu Kampuni yangu ya Msama Promotion mwaka huu inafanya onesho kubwa la miaka 15 tangu tuanze Tamasha la Pasaka, wadau wetu mbalimbali wamekuwa wakitoa maoni yao namna ya kuboresha na wamekuwa wakitutajia aina ya wasanii wanaotaka waje, idadi yao mpaka leo asubuhi (jana) imefikia 87, ni idadi kubwa ambayo haijapata kutokea kuombwa na mashabiki.
 
“Kati ya wasanii hao, 27 ni wa hapa nchini, 15 ni nchi nyingine za Afrika Mashariki , tisa Afrika Kusini, 14 sehemu nyingine za Afrika,  nane Uingereza na waliobaki ni kutoka Marekani,” alisema Msama.
 
Hata hivyo alisema kwa mazingira yaliyopo kamati yake haiwezi kuwaleta wasanii wote hao badala yake watakachofanya ni kukutana na kuteua wachache watakaokuja kutumbuiza kutokana na vigezo vyao.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...