Kwa moyo mkunjufu kabisa, nina penda kuwapongeza sana kituo cha radio cha 93.7 EFM kwa kutimiza mwaka mmoja tangu waanze kurusha matangazo yao hewani.
 Nina sababu nyingi za kuwapongeza lakini wakati wa kugonga “glass za cheers” niseme hivi; Kwanza kama unatafuta mifano halisi ya ufafanuzi wa mpango wa
serikali wa matokeo makubwa sasa (BRN) mimi nafikiri EFM ni mfano halisi.  
Kwa nini nasema hivi?   
Yaami ndani ya siku 365 tu, radio mpya imeweza kufikia nafasi ya pili kwa kusikilizwa na nakupendwa jijini Dar es salaam kwa mujibu wa kampuni ya utafiti ya Geo Poll. Lakini pia ukiangalia uongozi wa kituo hiki, ni vijana na kwa wastani umri wao ni miaka 35, huo ni mfano mzuri kwa vijana. 
Uongozi wa EFM kwanzia Mkurugenzi Mtendaji ni Francis Ciza (Majey), Geoffrey Ndawula, Dennis Ssebo, Dickson Ponela, Hamida Siu, Omar Ramathan na Reuben Ndege na hao wote ni vijana tunaoishi nao mtaani lakini wamethubutu na wameweza. 
Sababu nyingine ya kuwapongeza leo 93.7 EFM kwa kutimiza mwaka mmoja ni jinsi walivyo buni vipindi vyao na sio ku “copy na ku paste” Nani alijua kwamba michezo inaweza kurushwa hewani saa tatu asubuhi kila siku na kukubalika ? Sasa EFM wana sports headquarters kila Jumatatu hadi Ijuma, huu ni ubunifu na imekuwa ni changamoto sokoni.

Hongereni sana 93.7 EFM, 
na acha muziki uongee zaidi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hb day e fm,endelezeni maujanja maana sport head quarter kipindi cha michezo nina moja ya maujanja msiiachie hapo kila siku lazima mtuongozee maujanja,wapi mkude simba na dr panjuan bila kumsahau chogo chemba,I love this station.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...