Naibu Waziri wa Maji, Mh. Amos Makalla amefanya ziara ya kikazi wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma, pamoja na mambo mengine amezindua mradi mkubwa wa Maji katika kijiji cha Mkongo Nakawale ambapo watu zaidi ya 4000 wanapata Maji safi.

Aidha amekagua mradi wa Maji Milonji na ametoa agizo hadi kufikia tarehe mei 12 mwaka huu mkandarasi awe amekamilisha kuchimba kisima kingine baada ya kisima cha awali kuwa na Maji machache.

Amemwagiza Katibu Mkuu  wa Wizara ya Maji kuunda kikosi kazi cha watalaam kwenda Namtumbo kufuatilia matumizi ya Fedha kwa miradi ya Maji wilaya ya Namtumbo.
Naibu Waziri wa Maji Mh. Amos Makalla akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo, mara tu alipowasili kwenye Ofisi za Mkuu wa Wilaya hiyo kukagua na kuzindua miradi ya maji wilayani Namtumbo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Mh. Agnes Hokororo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...