Jana tarehe 29 Juni 2015, Mamlaka ya Bandari Tanzania imefungua rasmi Ofisi nchini Zambia. Ofisi hizo zimefunguliwa katika Jiji la Lusaka. 
 Dhumuni kubwa la Mamlaka ya Bandari kufungua ofisi hii Lusaka ni kutokana na kuwepo malalamiko kwa upande wa Zambia ambaye ni mteja wake mkubwa ya kuwepo ukiritimba wa utoaji wa mizigo yao bandarini Dar es salaam. 
Hivyo Mamlaka ikaona ni vema kuja kufungua ofisi jijini  Lusaka ili kutatua tatizo hilo. 
 Sherehe za ufunguzi wa ofisi hii ulihudhuriwa na Mhe Dkt. Charles Tizeba Naibu Waziri wa Uchukuzi na viongozi waandamizi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania. 
Ofisi za Mamlaka ya Bandari zipo katika Jengo la Ubalozi wa Tanzania Lusaka Zambia. Ofisi hii imefunguliwa rasmi na Waziri wa Uchukuzi wa Zambia Mhe Yamfwa Dingle Mukanga.
 KAIMU MKURUGENZI MKUU WA TPA  BW A. MASSAWE AKITOA HOTUBA WAKATI WA UFUNGUZI
 VIONGOZI WAANDAMIZI WAKIMSILIKIZA MHE. BALOZI AKITOA HOTUBA
 MHE GRACE J. MUJUMA BALOZI WA TANZANIA NCHINI ZAMBIA AKITOA HOTUBA WAKATI WA SHEREHE ZA UFUNGUZI

 MHE BALOZI NA MHE NAIBU WAZIRI WAKIKAGUA OFISI YA TPA NCHINI ZAMBIA KABLA YA UFUNGUZI
BALOZI WA TANZANIA NCHINI ZAMBIA MHE. BALOZI GRACE J. MUJUMA AKIWA NA MHE. NAIBU WAZIRI CHARLES TIZEBA UBALOZINI. MHE. TIZEBA ALIKWENDA KUMSALIMIA MHE. BALOZI OFISINI KWAKE.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...