Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikaribishwa na Mama Elizabeth Chatham, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Caniberra nchini Australia inayotoa huduma ya Afya ya Mama, vijana na watoto mara baada ya kufika eneo la hospitali kwa madhumuni ya kujionea namna bora yautoaji huduma.  Mama Salma yupo nchini Australia akifuatana na mumewe Rais Jakaya Kikwete kwenye ziara rasmi ya kiserikali nchni humo.
Mke wa Rais na Mama Salma Kikwete na mwenyeji wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya CaniberraMama Elizabeth Chatham wakibadilishana mawazo wakati walipokuwa wakitembelea maeneo mbalimbali ya kutolea huduma ya mama, vijana na watoto.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwaangalia baadhi ya watoto wanapatiwa huduma ya matibabu katika hospitali ya Caniberra wakijishughulisha na michezo mbalimbali wakiwa na wazazi wao.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Na Mwandishi wetu – Canberra, Australia 

Wafanyakazi wa Hospitali ya wanawake na watoto ya Centenary ya  mjini Canberra wameonyesha nia ya kufanya kazi nchini Tanzania ili kumuunga mkono Mke wa Rais Mhe. Mama Salma Kikwete katika juhudi zake za kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia afya za wanawake, vijana na watoto wa Hospitali hiyo Liz Chatham wakati akiongea na Mhe. Mama Kikwete na ujumbe wake walipotembelea Hospitali hiyo.
Liz  alimshukuru Mama Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) kwa kutembelea Hospitali hiyo na kujioneka kazi wanazozifanya pia alimpongeza kwa juhudi zake anazozifanya za kuhakikisha wanawake na watoto wa Tanzania wanapata huduma bora ya afya.

Mkurugenzi huyo alisema katika Hospitali hiyo wafanyakazi wengi  wa sekta ya afya wanapenda kwenda kufanya kazi Tanzania  ili waweze kutoa huduma ya afya kwa ajili ya mama na mtoto pamoja na watu wengine  na kubadilishana ujuzi wa kazi na wenzao.

Kwa upande wake Mhe. Mama Kikwete alisema  ni jambo la kufurahisha kuona katika Hospitali hiyo wanawake wenye afya njema wanajifungua katika mazingira mazuri na watoto ambao ni wagonjwa wanapewa matibabu na  uangalizi wa hali ya juu.

“Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kuwahudumia kinamama wajawazito na watoto, kujifungua iwe sababu ya kuwa na  furaha na kusherehekea lakini siyo tofauti na hapo, nasema hivi kutokana na mazingira halisi ya kule ninakotoka”.

Pamoja na kuwa jitihada za makusudi zinafanywa na Serikali bado wanawake na watoto wanapoteza maisha wakati wa kujifungua kutokana na sababu zinazoweza kuzuilika”, alisema Mama Kikwete.

Akiwa katika Hospitali hiyo Mama Kikwete alipata nafasi ya kuongea na watoto ambao ni wagonjwa  ambao kwa wakati huo walikuwa darasani wanasoma na aliwaona  na kuwajulia hali wazazi waliojifungua Hospitalini hapo.

Utaratibu wa Hospitali ya wanawake na watoto ya Centenary mtoto akiwa amelazwa kipindi ambacho shule hazijafungwa anafundishwa masomo ambayo wenzake wanafundishwa darasani kwani Hospitalini hapo kuna madarasa na walimu wanaofundisha watoto wagonjwa.

Mama Kikwete ameambatana na mmewe Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete nchini Australia kwa ajili ya ziara rasmi ya Kiserikali ya siku nne.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...