Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA), Bw. Dickson Mveyange (kulia) akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu tathmini ya ushiriki wa Viziwi kwenye Uchaguzi Mkuu wa Taifa Tanzania Bara uliofanyika 25 Oktoba, 2015. Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Jijini Dar es Salaam 24 Novemba, 2015. 
Mshauri Mwelekezi Elimu ya Uraia kwa Watu wenye Viziwi, Bw. Novath Rukwago (Kushoto) akijibu baadhi ya maswali toka kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu ushiriki wa Viziwi kwenye Uchaguzi Mkuu wa Taifa Tanzania Bara uliofanyika 25 Oktoba, 2015. Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Jijini Dar es Salaam 24 Novemba, 2015.
Baadhi ya Waandishi wa Habari toka Vyombo mbalimbali wakifuatilia taarifa toka kwa Viongozi wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) kuhusu tathmini ya ushiriki wa Viziwi kwenye Uchaguzi Mkuu wa Taifa Tanzania Bara uliofanyika 25 Oktoba, 2015. Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Jijini Dar es Salaam 24 Novemba, 2015.
(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO).

Na Zawadi Msalla
CHAMA Cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) kimeeleza masikitiko yao juu ya ushiriki mbovu wa Viziwi katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba kote nchini.

Akizungumza na waandishi wa Habari katika ukumbi wa Habari-MAELEZO leo mshauri mwelekezi wa elimu ya uraia kwa watu wenye ulemavu Novat Rukwago amesema licha ya jitihada mbalimbali ambazo walijaribu kuzifanya ili kuhakikisha viziwi kote nchini wanapata haki yao ya msingi na ya kikatiba ya kupiga kura bado ushiriki wao haukuridhisha.

Rukwago alizitaja changamoto mbalimbali zilizo jitokeza katika uchaguzi huo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa wataalamu wa lugha za alama zinazotumiwa na viziwi katika kampeni mbalimbali za Vyama vya Siasa, hivyo sera na Ilani za vyama hivyo hazikuweza kujulikana kwa viziwi.

“Vyama vingi vilisema ni suala la rasilimali na ukosefu wa fedha za kuweka wataalamu hao, ingawa tuonavyo sisi ni kwamba walishindwa kutoa kipaumbele na si suala la fedha,” alisema Rukwago.

Aidha, Rukwago alisema CHAVITA kwa juhudi binafsi waliweza kutembea jumla ya mikoa 17 kote nchini na kufanikiwa kutoa elimu kwa baadhi ya viziwi ambapo jumla ya viziwi 2516 walijiandikisha, idadi hiyo ikiwa na wanaume 1256 na wanawake 1260. Waliopiga kura walikuwa ni 1807.

Aliongeza kwa kusema kuwa licha ya changamoto hizo pia mazingira ya kupigia kura hayakuwa rafiki kwa watu wenye uhitaji maalumu kwani hakukuwa na wataalamu wa lugha za alama katika vituo vya kupigia kura.

Waliiomba Serikali kuzingatia umuhimu wa kuyapa kipaumbele makundi mbalimbali yenye uhitaji kwa chaguzi zijazo na kuitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kufanya mawasiliano na vyama vya watu wenye uhitaji maalum mapema ili kuweza kushirikiana katika kuondoa changamoto zilizojitokeza katika uchaguzi wa mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...