MWIMBAJI maarufu wa muziki wa Injili Tanzania, Upendo Nkone naye amejitokeza kuwa mmoja wa waimbaji watakaofikisha ujumbe wa Shukrani kwa Mungu katika Sikukuu ya Krismasi kupitia tamasha linalotarajia kufanyika Desemba 25 mwaka huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama Kamati imefanikisha makubaliano na mwimbaji huyo.Msama alisema Nkone anaungana na wenzake Rose Muhando, Ephraim Sekeleti sambamba na Kwaya ya Wakorintho wa pili.

"Kabla ya kukubaliana na Nkone, tulikuwa tumeshamalizana na wenzake Rose Muhando, Ephraim Sekeleti ambaye ni raia wa Zambia sambamba na Kwaya ya Wakorintho wa Pili yenye maskani yake Mafinga mkoani Iringa, bado tunaendelea na mawasiliano na waimbaji wengine ili kunogesha tamasha hilo lenye malengo mawili ambayo ni Shukrani kwa Mungu sambamba na Sherehe za kuzaliwa Masiha, Yesu Kristo," alisema Msama.

Aidha Msama alisema Kamati yake imepanga kufikisha shukrani kwa Mungu kupitia waimbaji na viongozi wa dini na wa kada mbalimbali kama ilivyokuwa kwenye Tamasha la Kuombea Amani lililofanyika Oktoba 4 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambako mgeni rasmi alikuwa ni mke wa rais wa awamu ya nne, Salma Kikwete.

"Oktoba 4, tuliandaa Tamasha la kumbea amani uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 uwanja wa Taifa, hivyo ni nafasi yetu kumshukuru Mungu baaada ya kupitisha Tanzania kwenye uchaguzi ambao ulikuwa na viashiria vya uvunjifu wa amani," alisema Msama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...