"Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limewaonya viongozi wa vilabu, wachezaji, waamuzi na wasimamizi wa mchezo kutojihusisha na upangaji wa matokeo (Match fixing) katika michezo inayoendelea sasa katika ligi za ngazi mbalimbali za nchini" amesema Baraka Kizuguto msemaji wa TFF (Pichani). 

 Kizuguto amesema TFF imejipanga na inasimamia vizuri michezo ya Ligi Kuu (VPL), Daraja la Kwanza (FDL), Daraja la Pili (SDL) na Azam Sports Federation Cup (ASFC) inayoendelea na yoyote atakayebainika kujihusisha na mchezo huo wa upangaji matokeo, hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa. 

"Katika michezo yote inayoendelea TFF ina maofisa wake wanaofuatilia kwa ukaribu michezo hiyo, hivyo endapo kiongozi, mchezaji, msimamizi au mwamuzi atabainika kujihusisha na upangaji wa matokeo hatua kali zitachukuliwa", amesema Kizuguto, akiongezea kuwa  TFF inawaomba viongozi, wachezaji, wasimamizi wa michezo na waamuzi kutojihusisha na mchezo huo wa upangaji wa matokeo kwani kufanya hivyo ni kukiuka katiba, sheria na kanuni zinaongoza mpira wa miguu nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...