Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, amesema mkoa wake umepokea Tani 500 za Sukari, zikitokea
kiwanda cha sukari cha Kagera Sugar tarehe 24, Mei, 2016, ambazo zinaingizwa
mkoani hapo na muagizaji na Msambazaji P.H Shah.
Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa ameonya watu watakao uza sukari hiyo kinyume na bei
elekezi , na kusema kuwa watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa nipamoja nakufikishwa katika
vyombo vya dola.
Mongella amesema pia kwamba, kupitia kamati yakushughulikia sukari, tayari
wametoa maelekezo kwa Wakuu wa wilaya jinsi yakushughulikia suala la sukari
na kwamba wasambazaji wote katika Wilaya lazima wazingatie maelekezo bila
kuvunja utaratibu utakao wekwa.
Mahitaji ya sukari katika mkoa wa Mwanza ni Tani 1,500 kwa wiki kwa matumizi
ya kawaida kwa wananchi wake, hivyo kuwasili kwa tani 500 ukweli kwamba
itasaidia kupunguza uhaba wa sukari unao ukabili mkoa huu kwa sasa.
Hata hivyo mkuu wa mkoa amewatoa wanachi hofu juu ya sukari kwakusema,
tayari viwanda vya hapa nchini vimekwisha anza uzalishaji wa sukari na kwamba
muda si mrefu tatizo la sukari litapungua kama sio kuisha kabisa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...