Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Studio ya Radio ya Jamii iliyopo katika Chuo Kikuu Huria nchini (OUT), Kinondoni Jijini Dar es salaam  Juni 27, 2016.  Kulia ni Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akifuatiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elias Bisanda. Studio hiyo ni moja kati ya Studio nyingi za Radio za Jamii zilizopo maeneo mbali mbali hapa nchini, zinazodhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana na Mtandao wa Radio za Jamii Tanzania (COMNETA). 
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akizungumza katika kipindi cha moja kwa moja cha Redio ya Jamii iliyopo katika Chuo Kikuu Huria nchini (OUT), mara baada ya kuifungua rasmi Studio hiyo, Kinondoni Jijini Dar es salaam  Juni 27, 2016. Kulia kwake ni Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akifuatiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elias Bisanda.
Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues, akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya ufunfunguzi wa Studio Studio ya Radio ya Jamii iliyopo katika Chuo Kikuu Huria nchini (OUT), Kinondoni Jijini Dar es salaam  Juni 27, 2016.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elias Bisanda akizungumza wakati wa hafla ya ufunfunguzi wa Studio Studio ya Radio ya Jamii iliyopo katika Chuo Kikuu Huria nchini (OUT), Kinondoni Jijini Dar es salaam Juni 27, 2016.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...