Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kagera

MWENYEKITI wa Bodi ya mfuko wa Taifa wa bima ya afya(NHIF) Anne Makinda amesema kuwa kituo chochote kilichosajiliwa kwa ajili ya kutoa huduma ya afya kwa wateja wa mfuko wa bima ya afya, ambacho kimeajiri wahudumu wenye mfumo wa unyanyasaji kwa wagonjwa ikiwemo Lugha za kejeli kwa wateja vitaondolewa kwenye mpango wa huduma ya afya.

Makinda alisema hayo leo wakati wa mkutano wa wadau wa NHIF na CHF Mkoani Kagera katika ukumbi wa mikutano wa mkuu wa mkoa wa Kagera Mjini Bukoba.

"Hivi wewe mtoa huduma wa afya unapotoa lugha ya kejeli na vitisho,matusi kwa wagonjwa unapata faida gani?,unapata fedha kiasi gani?sasa naagiza vile vituo ambavyo tumevisajiri kutoa huduma zetu ambavyo bado vinaendekeza mfumo wa kunyanyasa wagonjwa, sasa tunasema basi hatuwezi kuvumilia kinachofuata kuwafuatia sajili alisema Makinda.

Aidha aliwaagiza wamiliki wa vituo hivyo kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja kuweka mkakati madhubuti wa kuhakikisha wanaondoa kero hiyo haraka iwezekanavyo kwani watu wakijiunga na bima lengo ni wapate huduma stahiki ikiwemo mapokeo mazuri jambo ambalo linampa mgonjwa faraja hata kabla ya kupata dawa.

Mwenyekiti wa bodi ya mfuko wa bima ya afya Taifa(NHIF)Anna Makinda akifungua mkutano wa wadau wa mfuko wa bima ya afya Mkoa wa Kagera katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Kaimu Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa bima ya afya(NHIF)Benard Konga akiongeo na wadau wa mfuko huo(hawapo pichani)wakati wa kikao cha wadau wa mfuko wa NHIF kilichofanyika leo Mkoani Kagera

Meneja wa mfuko wa bima ya afya(NHIF)Mkoa wa Kagera Elias Odhiambo akieleza changamoto na mafanikio ya mfuko katika Mkoa wa kagera kwa wadau wa mfuko wa Bima. 


Baadhi ya wadau wa mfuko wa bima ya afya wa Mkoa wa Kagera wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa mkutano wa wadau wa bima ya afya na viongozi kutoka makao makuu ya mfuko huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...